Na Mwandishi wetu- Kibaha, Pwani
Halmashauri ya Manispaa ya Kibaha kupitia idara ya afya imetoa mafunzo kwa wahudumu wa afya ngazi ya jamii na kufanya tathmini ya magonjwa yasiyoambukiza na namna ya kukabiliana nao.Mafunzo hayo yametolewa na Wizara ya Afya kupitia taasisi ya TANCDA inayojihusisha na utoaji wa elimu kwa umma juu ya magonjwa yasiyoambukiza na namna ya kupambana nayo ikiwemo kubadilisha mtindo wa maisha.
Mratibu kitengo cha magonjwa yasiyoambukiza kutoka Wizara ya Afya Dkt Grace Gembe amesema magonjwa yasiyoambukiza yamekuwa kwa kasi sana ni muhimu sana wananchi waweze kupata uelewa na elimu ili kujilinda.
Gembe amesema, anaamini mafunzo haya yatakuwa na tija kwa wahudumu hawa wa ngazi ya jamii ambapo watakaporudi kwenye mitaa yao watakuwa walimu wazuri kwenye kuelemisha jamii.
Kwa upande wa Mganga Mkuu Halmashauri ya Manispaa ya Kibaha Dkt Catherine Saguti amesema kwa siku ya leo wametoa mafunzo kwa vijana 40 ila wanajumla ya vijana 135 katika mitaa yote 73 ya Manispaa ya Kibaha.
Amesema, vijana hao wote watapata mafunzo ya namna ya kutoa elimu kwa jamii juu ya magonjwa yasiyo yakuambukiza katoka ngazi ya jamii na namna ya kukabiliana nayo.
Baada ya kumalizika kwa mafunzo hayo, vijana hao wamepatiwa kitabu kinachoelezea magonjwa mbalimbali yasiyoambukiza na namna ya kujitambua pindi unapokuwa na dalili zilizoanishwa humo.


Toa Maoni Yako:
0 comments: