Mbunge wa Mikumi kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) ambaye pia ni Msanii wa Muziki wa Kizazi kipya Joseph Haule a.k.a Profesa Jay (kulia) amepata pigo la kufiwa na baba yake mzazi (kushoto) leo akiwa katika Hospitali ya St. Kizito, Mikumi, ambapo alikuwa asafirishwe kwenda kupata matibabu zaidi Hospitali ya Taifa ya Muhimbili.

Mhe. Joseph Haule amethibitisha kifo hicho katika mawasiliano aliyoyafanya kwa njia ya simu akiwa Dodoma.

Aidha viongozi mbalimbali kupitia kurasa zao za mitandao ya kijamii wametoa salamu zao za pole kwa Mbunge huyo na kumwombea kwa Mungu amtie nguvu katika kipindi hiki kigumu.

KAJUNASON BLOG inatoa pole kwa wafiwa.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: