Mjukuu wa Malkia wa Uingereza Elizabeth II Prince William aakiwa na faru alipotembelea hifadhi ya Mkomazi iliyopo mkoani Tanga akiwa katika ziara yake ya siku nne nchini.
Mjukuu wa Malkia wa Uingereza Elizabeth II Prince William akiwa mwenye furaha baada ya kushuhudia ongezeko la faru alipotembelea hifadhi ya Mkomazi iliyopo mkoani Tanga akiwa katika ziara yake ya siku nne nchini.
---

Mjukuu wa Malkia wa Uingereza Elizabeth II Prince William ametembelea hifadhi ya Mkomazi iliyopo Tanga na hii ni katika ziara yake ya siku 7 kwa nchi za Tanzania, Kenya na Namibia. 


Akiwa katika hifadhi hiyo Prince alifanikiwa kujionea namna faru weusi wanavyolindwa na kuongezeka zaidi, ambapo imeelezwa kuwa aina hiyo ya wanyama hupungua kutokana na ujangili na ongezeko la watu nchini. 


Pia amejifunza namna faru hao wanavyoongezeka kwa kuzaliana na hadi sasa kuna takribani ya faru wasiopungua 50 katika hifadhi hiyo na wataalamu mbalimbali wamesema kuwa wanapiga vita na kuimarisha sekta ya ulinzi ili kuweza kukomesha ujangili unaopunguza wanyama mbugani. 

Prince Willium ametembelea Tanzania na baadhi ya nchi za Afrika akiwa Rais wa mashirika yanayotetea uhifadhi wa wanyama ya "United for Wildlife" na "Tusk Trust" na akiwa nchini alipokelewa Ikulu na Rais Dkt. John Magufuli na Waziri wa Maliasili na Utalii Dkt. Hamis Kigwangala.

Aidha katika ziara hiyo katika hifadhi hiyo Prince ameshuhudia namana watoto wanavyopewa elimu kuhusiana na utunzaji wa wanyama na baadaye kujiunga katika timu za ulinzi kwa wanyama.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: