Nikiwa kama baba wa kiroho na mlezi mkuu wa waimbaji wote wa nyimbo za injili Tanzania, napenda kuweka wazi kuwa nimehuzunishwa sana na hii video ya maombezi ya muimbaji mwenzetu Rose Muhando.

Kwa unyenyekevu kabisa naweza kusema kuwa, maombi ni muhimu sana kwa watu wote, ila namna ya kuombea ikiwa mbaya inaweza kuharibu umuhimu wote wa maombi na kusababisha maombi yadharaurike au yamdharaulishe aliyeombewa.

Katika nia yangu ya ndani nimefurahishwa sana na kitendo cha Rose kuombewa, ila kero yangu kubwa imekuwa kwenye njia iliyotumika kumuombea.

Rose Muhando ni star, na katika medani za mziki wa injili ni mtu anaetazamwa na watu wengi sana kama rol model wao, hivyo nadhani ilikuwa ni bora zaidi kuwa waangalifu katika kumuombea ili kulinda brand yake.

Biblia inasema, mwenye heshima apewe heshima, hivyo kwangu mimi sidhani kama mchungaji aliyemuombea Rose amempatia heshima anayostahili, maana binafsi sikuona haja ya kuwasha camera na kuanza kumuombea hadharani vile.

Hali hii inaweza kumtangaza sana muombeaji lakini kwa upande wa muombeaji inaweza kuzidisha tatizo na kusababisha adharaulike zaidi kwenye jamii inayomtazama.

Watumishi wa Mungu wanahitaji kuwa na hekima pamoja na kifua cha kutunza siri, na siyo kufanya mambo kwa mihemko huku mkitazama maslahi yenu. Mimi nadhani ingekuwa bora sana endapo mchungaji angemuombea ofisini, na kama maombi yangeleta majibu naamini video ya shuhuda ambayo Rose Muhando angeongea wakati akiwa na akili zake timamu ndiyo ingefaa kusambaa na kuendelea kumjengea heshima yeye pamoja na mtumishi aliyemuhudumia.

Kumbuka yule akida (mkuu wa vikosi cha askari wa kirumi) alipohitaji maombi kwa Yesu, biblia inasema Yesu alifunga safari kwenda nyumbani kwake ili kumuombea. Unadhania ni kwanini hakumwambia alete askari wake mgonjwa amuombee hadharani kama akina Batromayo? Hii ilikuwa ni hekima ya kulinda heshima ya muombewaji. Maana huwezi kumuombea raisi kama unavyoombea ombaomba au mpiga debe!

Kwa kweli nimeamua kuwa muwazi na kuziweka huzuni zangu hadharani ili waombeaji mjirekebishe. Siyo kila maombi yafanyike wakati kamera zimewashwa (ON), kuna mengine ya kuzima kamera na kuomba kwa staha ili kuendeleza uhai wa kipawa au heshima aliyo nayo huyo unaemuombea.

RAISI WA MAKAMANDA WA YESU
KONKI MASTER WA GOSPEL
BALOZI WA AMANI TANZANIA

HII NDIYO VIDEO ALIYOKUWA AKIOMBEWA MWIMBAJI ROSE MUHANDO.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: