Articles by "HABARI ZA KIJAMII"
Showing posts with label HABARI ZA KIJAMII. Show all posts
Mkurugenzi wa Vodacom Business Nguvu Kamando, akizungumza na waandishi wa habari kuhusu msimu mpya wa msafara wa Nyerere Cycling Tour (zamani Twende Butiama) utakaozinduliwa mnamo mwezi wa kumi ukiambatana na mashindano ya mbio za Vodacom Coastal Classic.
Wadau na Washiriki wa msafara wa mbio za Nyerere Cycling Tour (zamani Twende Butiama) wakipiga makofi kama ishara ya kufurahia ujio wa mashindano ya mbio za Vodacom Coastal Classic.
Mwanzilishi wa Msafara wa Mbio za Twende Butiama, Gabriel Landa akizungumza na waandishi wa habari kuhusu msimu mpya wa msafara wa Nyerere Cycling Tour (zamani Twende Butiama) utakaozinduliwa mnamo mwezi wa kumi.
Wadau wa msafara wa Cycling tour (zamani Twende Butiama) wakisikiliza kwa makini kuhusu msimu mpya wa msafara huo na ujio wa Mashindano ya Vodacom Coastal Classic utakaozinduliwa mnamo mwezi wa kumi mwaka huu.

Na Mwandishi Wetu.

>Msimu mpya kuanza Oktoba ukitanguliwa na Vodacom Coastal Classic

>Ni mashindano ya mbio za baiskeli za km 109 kutoka Dar hadi Bagamoyo

Dar es Salaam, Tanzania, 6 Agosti 2026: Katika hatua muhimu kwa maendeleo ya mchezo wa kuendesha baiskeli nchini Tanzania, Vodacom Tanzania Plc kwa kushirikiana na Chama cha Baiskeli Tanzania (CHABATA), leo imetangaza rasmi kubadilishwa kwa jina la msafara wa baiskeli wa Twende Butiama na kuwa Nyerere Cycling Tour, huku pia wakitangaza kuzindua mashindano mapya ya mbio za baiskeli za kilomita 109 za Vodacom Coastal Classic, zinazolenga kuiweka Tanzania kwenye ramani ya kimataifa ya mashindano ya baiskeli.

Tangu kuanzishwa kwake mwaka 2016, msafara huu umekuwa ukienzi urithi wa kudumu wa Mwalimu Julius K. Nyerere kwa kuendeleza fursa sawa kwa wote kupitia uboreshaji wa mazingira ya kujifunzia, ujenzi wa miundombinu ya vyoo, pamoja na kuchangia vifaa vya kuwawezesha wanafunzi wenye mahitaji maalum ili kila mtoto aweze kupata fursa ya elimu.Hadi sasa, msafara huo umefikia zaidi ya shule 107 na kuboresha maisha ya wanafunzi zaidi ya 75,000 wanaofaidika kupitia ujenzi wa madarasa bora na jumuishi yanayokidhi mahitaji ya wanafunzi wote.

Vodacom Tanzania Foundation ilianza kushirikiana na CHABATA kufadhili msafara huu miaka mine iliyopita, na katika kipindi hicho msafara wa Twende Butiama umekuwa mara nne zaidi, huku ukivutia washiriki kutoka Tanzania, ukanda wa Afrika Mashariki na kimataifa. Msafara wa mwaka huu utafanyika kuanzia tarehe 5 hadi 14 Oktoba 2026, washiriki wakianzia Bagamoyo hadi Butiama.

Ili kuakisi dhamira kuu ya msafara huu unaoenzi urithi wa Mwalimu Nyerere huku ndani yake wakipanga kuyawezesha kukua ili kuwa mashindano ya kimataifa ya baiskeli, kuanzia mwaka huu msafara huu utajulikana rasmi kama Nyerere Cycling Tour.

Dhamira ya mwaka huu ni moja: kukuza mchezo wa baiskeli na kuiweka Tanzania katika ramani ya kimataifa ya mchezo wa baiskeli. Kwa kushirikiana na CHABATA, Vodacom Tanzania inazindua mashindano makubwa ya baiskeli ya Vodacom Coastal Classic, yakihusisha mbio za kilomita 109 zitakazoshirikisha waendesha baiskeli wa kiume na wa kike.

Mbio hizi zitaanzia Dar es Salaam, kuelekea kaskazini hadi Makurunge mkoani Pwani na kumalizikia katika eneo la kihistoria la Old Boma, Bagamoyo, zikikamilisha safari ya kilomita 109. Kwa mara ya kwanza mashindano haya yatafanyika Jumapili, tarehe 4 Oktoba 2026, siku moja kabla ya kuanza kwa msafara wa baiskeli wa Nyerere Cycling Tour. Baada ya hapo, Vodacom Tanzania itaendesha mashindano haya kila mwaka ifikapo Jumapili ya kwanza ya mwezi Oktoba.

Kwa mara ya kwanza, washiriki zaidi ya 400 kutoka Tanzania na mataifa mbalimbali duniani wanatarajiwa kushiriki katika mbio hizi, "Tunataka kukuza mchezo huu," alisema Nguvu Kamando, Mkurugenzi wa Vodacom Business. "Kila siku tunaona waendesha baiskeli kwenye barabara zetu, aidha wakiwa ni wataalamu au washiriki wa kawaida. Hakuna sababu kwa nini Abella kutoka Mwanza asiweze kushindana hapa Tanzania na kwenye majukwaa ya kimataifa, au Saidi kutoka Shinyanga. Wanachohitaji ni vifaa sahihi na mafunzo sahihi. Vodacom Coastal Classic inalenga kuhamasisha na kuwapa motisha Watanzania wengi zaidi kuingia katika mchezo huu."

Gabriel Landa, Mwanzilishi wa Nyerere Cycling Tour, alisema, "Nyerere Cycling Tour imekuwa zaidi ya msafara wa baiskeli. Ni kuhusu kuendeleza maono ya Mwalimu Nyerere ya heshima na fursa sawa kwa kila Mtanzania. Kubadilisha jina la mashindano haya kwa heshima yake, sambamba na kuanzisha mbio za kiwango cha kimataifa za Vodacom Coastal Classic, ni mwanzo wa safari mpya. Tunajenga jukwaa ambalo vipaji vya Watanzania vinaweza kuibuka na kuvutia waendesha baiskeli kutoka kote duniani kuja kushiriki.

Tarehe Muhimu

Vodacom Coastal Classic (Mashindano ya kilomita 109): Jumapili, 4 Oktoba 2026 — Dar es Salaam hadi Makurunge, zikimalizikia Old Boma, Bagamoyo.

Nyerere Cycling Tour: Tarehe 5–14 Oktoba 2026 — Bagamoyo hadi Butiama.
Na Mwandishi Wetu, Dodoma

Waziri Mkuu Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Mizengo Pinda, ameshangazwa na kiwango cha ubunifu wa teknolojia zinazobuniwa na kuzalishwa na kampuni ya Mati Technologies baada ya kutembelea banda la kampuni hiyo katika Maonesho ya 33 ya Kitaifa ya Kilimo (Nane Nane 2026) yanayoendelea katika Viwanja vya Nzuguni, jijini Dodoma.

Mhe. Pinda alitembelea banda hilo leo na kupokea maelezo kutoka kwa viongozi na wataalamu wa Mati Technologies kuhusu shughuli mbalimbali zinazofanywa na kampuni hiyo katika kubuni na kutengeneza teknolojia zinazolenga kuongeza tija katika sekta ya kilimo na maeneo mengine ya maendeleo.

Katika ziara hiyo, alikagua teknolojia mbalimbali zinazotengenezwa na kampuni hiyo, ikiwemo ndege nyuki zinazotumika kunyunyiza viuatilifu na mbolea mashambani kwa usahihi, haraka na ufanisi mkubwa, pamoja na mifumo mingine ya kisasa ya kiteknolojia inayolenga kuboresha uzalishaji wa kilimo.

Baada ya kushuhudia namna teknolojia hizo zinavyofanya kazi, Mhe. Pinda alisema ameridhishwa na hatua kubwa ya ubunifu iliyofikiwa na wataalamu wa Kitanzania.
“Ni jambo la kujivunia kuona Watanzania wakibuni na kuzalisha teknolojia za kisasa zinazotoa suluhisho kwa changamoto mbalimbali za maendeleo, hususan katika sekta ya kilimo,” alisema.

Alisema maendeleo hayo yanaonesha uwezo mkubwa wa wataalamu wa ndani katika kubuni teknolojia zinazokidhi mahitaji ya nchi na kuchangia kukuza uchumi kupitia sekta ya kilimo na viwanda.
Aidha, aliipongeza Mati Technologies kwa kuwekeza katika utafiti, ubunifu na uzalishaji wa teknolojia za ndani, akisisitiza kuwa juhudi hizo zinapaswa kuungwa mkono ili kuharakisha maendeleo ya taifa na kuongeza ushindani wa bidhaa za Kitanzania katika soko la ndani na kimataifa.

Kwa upande wake, uongozi wa Mati Technologies ulisema kampuni itaendelea kubuni na kuzalisha teknolojia zenye ubora wa hali ya juu zitakazorahisisha shughuli za uzalishaji, kuongeza tija kwa wakulima na kuchochea matumizi ya teknolojia katika sekta mbalimbali za uchumi.
Maonesho ya Nane Nane yameendelea kuwa jukwaa muhimu la kuonesha mafanikio ya sekta za kilimo, mifugo, uvuvi, viwanda na teknolojia, huku yakivutia maelfu ya wananchi, wakulima, wawekezaji, wanafunzi na wataalamu kutoka maeneo mbalimbali nchini.

Kupitia ubunifu wa teknolojia zinazozalishwa hapa nchini, Mati Technologies inaendelea kujijengea sifa kama moja ya kampuni zinazochochea matumizi ya sayansi, teknolojia na utafiti katika kuongeza tija ya uzalishaji na kuchangia maendeleo endelevu ya Tanzania.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan akisalimiana na Rais wa Jamhuri ya Uganda Mhe. Yoweri Kaguta Museveni baada ya kuwasili katika viwanja vya Ikulu Jijini Dar es Salaam, tarehe 06 Agosti, 2026.
 Rais wa Jamhuri ya Uganda Mhe. Yoweri Kaguta akisaini Kitabu cha wageni, baada ya kuwasili katika viwanja vya Ikulu Jijini Dar es Salaam, tarehe 06 Agosti, 2026. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan akimpigia makofi Rais wa Jamhuri ya Uganda Mhe. Yoweri Kaguta Museveni baada ya kusaini Kitabu cha wageni katika viwanja vya Ikulu Jijini Dar es Salaam, tarehe 06 Agosti, 2026.

 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan akiwa kwenye picha na Rais wa Jamhuri ya Uganda Mhe. Yoweri Kaguta Museveni baada ya kuwasili katika viwanja vya Ikulu Jijini Dar es Salaam, tarehe 06 Agosti, 2026.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan akiwa kwenye mazungumzo na Rais wa Jamhuri ya Uganda Mhe. Yoweri Kaguta Museveni baada ya kuwasili katika viwanja vya Ikulu Jijini Dar es Salaam, tarehe 06 Agosti, 2026.
 Waziri wa Nishati wa Tanzania Mhe. Deogratius Ndejembi akizungumza kwenye mkutano wa Waandishi wa Habari baada ya hafla ya utiaji saini Hati ya Makubaliano kuhusu mapendekezo ya kuendeleza Tanga kama Kituo cha Nishati cha Kikanda ulioshuhudiwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan na Rais wa Jamhuri ya Uganda Mhe. Yoweri Kaguta Museveni, Ikulu, jijini Dar es Salaam, tarehe 06 Agosti, 2026.
 Waziri wa Nishati na Maendeleo ya Madini Mhe. Dkt. Musenero Masanza wa Uganda akizungumza kwenye mkutano wa Waandishi wa Habari baada ya hafla ya utiaji saini Hati ya Makubaliano kuhusu mapendekezo ya kuendeleza Tanga kama Kituo cha Nishati cha Kikanda ulioshuhudiwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan na Rais wa Jamhuri ya Uganda Mhe. Yoweri Kaguta Museveni, Ikulu, jijini Dar es Salaam,
tarehe 06 Agosti, 2026.


Rais Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akutana na Kuzungumza na Rais wa Jamhuri ya Uganda Mhe. Yoweri Kaguta Museveni, Ikulu Jijini Dare es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan na Rais wa Jamhuri ya Uganda Mhe. Yoweri Kaguta Museveni wakishuhudia utiaji saini Hati ya Makubaliano kuhusu mapendekezo ya kuendeleza Tanga kama Kituo cha Nishati cha Kikanda katika viwanja vya Ikulu, jijini Dar es Salaam, tarehe 06 Agosti, 2026. Hati hiyo ya Makubaliano imesainiwa kati ya Shirika la Maendeleo la Petroli Tanzania (TPDC) chini ya Mkurugenzi Mtendaji Bw. Mussa Makame, Kampuni ya Taifa ya Mafuta ya Uganda (UNOC) chini ya Mkurugenzi Mtendaji Bi. Proscovia Nabbanja pamoja na Kampuni ya Biashara ya Mafuta na Nishati ya Vitol ya Bahrain, chini ya Mkurugenzi Mtendaji wake Tom Baker.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan na Rais wa Jamhuri ya Uganda Mhe. Yoweri Kaguta Museveni wakishuhudia utiaji saini Hati ya Makubaliano kuhusu mapendekezo ya kuendeleza Tanga kama Kituo cha Nishati cha Kikanda katika viwanja vya Ikulu, jijini Dar es Salaam, tarehe 06 Agosti, 2026.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan akiagana na Rais wa Jamhuri ya Uganda Mhe. Yoweri Kaguta Museveni mara baada ya kuhitimisha ziara rasmi ambapo walishuhudia utiaji saini Hati ya Makubaliano kuhusu mapendekezo ya kuendeleza Tanga kama Kituo cha Nishati cha Kikanda kuwasili katika viwanja vya Ikulu Jijini Dar es Salaam, tarehe 06 Agosti, 2026.


Na Mwandishi Wetu, Dodoma

Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Hamad Chande, amefurahishwa na uelewa mkubwa ulioonyeshwa na wanafunzi waliopata elimu ya vipimo katika banda la Wakala wa Vipimo - (WMA), kwenye Maonesho ya 33 ya Wakulima Nane Nane.

Akizungumza leo Agosti 6, 2026 baada ya kuzungumza na wanafunzi hao aliowakuta katika Banda la WMA, Viwanja vya Dkt. John Malecela Nzuguni, Dodoma, Naibu Waziri ambaye pia alikuwa katika ziara ya kutembelea mabanda mbalimbali ya Maonesho, alisema ni hatua nzuri kwa WMA kuanza kuwafundisha watoto umuhimu wa vipimo sahihi wakiwa wadogo.

“Nimefurahishwa sana. Watoto hawa wameelewa kuwa kipimo sahihi ni haki ya kila mtu. Hawa ndio Maafisa Vipimo wa kesho,” alisema.

Awali, Naibu Waziri Chande alipowakuta wanafunzi hao bandani aliwauliza maswali mbalimbali kuhusu vipimo na waliweza kujibu kwa ufasaha.

Wanafunzi hao wa Shule ya Msingi Blessed Mabuba iliyopo jijini Dodoma, ambao waliongozana na mwalimu wao Irene Ketta, ambaye pia alipongeza WMA kwa kujielekeza katika utoaji elimu ya vipimo mashuleni hatua ambayo alisema imewawesha wanafunzi kueleza tofauti ya kipimo sahihi na kisicho sahihi, umuhimu wa kusoma lebo na jinsi ya kutumia mizani.

“Niwape pongezi WMA. Kama tutaendelea kuwapa elimu hii watoto wetu, tunajenga Taifa la wafanyabiashara waaminifu na walaji wenye ufahamu. Huu ndio msingi wa uchumi imara,” alisema Mwalimu Ketta.

WMA imeahidi kuhakikisha elimu ya vipimo inaenea kwa jamii nzima kupitia utoaji elimu kwa makundi mbalimbali wakiwemo wanafunzi.
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Dkt. Charles Msonde, ameupongeza Wakala wa Ufundi na Umeme Tanzania (TEMESA) kwa maboresho makubwa ya utoaji wa huduma, hususan matumizi ya teknolojia yanayorahisisha upatikanaji wa huduma kwa wananchi.

Dkt. Msonde amesema hayo leo, Agosti 5, 2026, alipotembelea banda la TEMESA katika Maonesho ya 33 ya Kitaifa ya Kilimo (Nane Nane 2026) yanayoendelea katika Viwanja vya Nzuguni, jijini Dodoma.
Dkt.Msonde Amesema kuwa ameridhishwa na maendeleo makubwa yaliyofikiwa na TEMESA, akieleza kuwa uimarishaji wa huduma za kidijitali pamoja na ongezeko la ubora wa mafundi umeongeza ufanisi wa wakala huo.

“Kilichonifurahisha zaidi ni uimarishaji wa mafundi. Sasa wanafanya kazi kwa weledi mkubwa na wanatengeneza magari kwa ubora. Kwa kweli TEMESA mmenifurahisha sana,hongereni sana” amesema Dkt. Msonde.
Aidha, amesema Serikali na wananchi wanaiamini TEMESA kutokana na mchango wake katika kulinda usalama wa magari ya Serikali na kuhakikisha matumizi sahihi ya fedha za umma. Amewataka viongozi na watumishi wa wakala huo kuendelea kubuni na kuboresha huduma kwa kutumia teknolojia.
Kwa upande wake, Meneja Masoko na Uhusiano kwa Umma- TEMESA, Bi. Martha Joachim, amesema miongoni mwa maboresho yaliyofanywa ni kuhuisha huduma ya ukodishaji wa mitambo kupitia Mfumo wa TIMIS, ambapo wateja sasa wanaweza kuwasilisha maombi ya ukodishaji kwa njia ya kidijitali, hatua iliyopunguza urasimu na muda wa kupata huduma.
Maonesho hayo yenye kauli mbiu “Tambua Soko, Ongeza Tija Kutekeleza Dira 2050”, yanatarajiwa kuadhimishwa tarehe 8 Agosti, 2026.