Meneja Mawasiliano wa shirika la Ndege la Fastjet, Lucy Mbogoro (mwenye nguo ya manjano) na Rubani wa shirika hilo wakiwa na Madaktari wa Chama cha Afya ya Meno na Kinywa Tanzania TDA kuelekea Mkoa Mara kutoka Dar ss Salaam kutoa huduma ya meno na kinywa bure kwa wagonjwa waliopo Butiama. Shirika la Fastjet lilitoa huduma ya usafiri kwa madaktari hao bure kwa siku tano ikiwa ni sehemu ya sherehe ya kutimiza miaka ya sita ya huduma za Fastjet Tanzania
---
Shirika la ndege la Watanzania wote na mshindi wa Tuzo mbalimbali inafuraha kudhamini usafiri wa ndege wa muda ya miaka minne sasa kwa Chama cha watoa huduma ya kinywa na meno Tanzania (TDA) na zaidi ya madaktari 20 pamoja na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamiii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mhe. Ummy Mwalimu kwa ajili ya kutoa huduma ya afya ya meno kwa mamia ya watu Mjini Butiama wakati wa kongamano ya 33 la wanasayansi wa huduma za afya ya meno.

‘Kama sehemu ya utowaji wa huduma kwa jamii, Fastjet inafuraha kubwa kuweza kutoa marejesho kwa jamii wakati tukisheherekea miaka 6 ya utoaji wa huduma ya anga Tanzania’. Haya yalisemwa na Mwenyekiti Mtendaji wa Fastjet Lawrence Masha ambaye pia alisema” Ni heshima kubwa kuweza kubadilisha maisha ya watoto na jamii kwa ujumla kwa kutoa huduma ya usafiri wa anga kwa madaktari ambao ni watalaam kutoka hospitali ya Muhimbili iliopo Dar es salaam kwenda Mwanza kutoa huduma ya afya ya meno kwa watoto pamoja na watu wengine ambao hawawezi gharama ya kusafiri kwenda Dar es salaam kwa matibabu.’

‘Fastjet inaendelea kutimiza ahadi yake kwa Wateja kwa kutoa huduma bora zaidi kwa gharama nafuu. ‘Hivi karibuni tulizindua huduma mpya ambayo Wateja wote wanaosafari na fastjet wanapata viburudisho bure kwenye ndege zetu pamoja na uzito wa kilo 23 ya mizigo unaoingizwa ndani na kilo 23 ya mzigo unaobebwa mkononi’. Aliongezea Ndugu Masha.

‘Tumeweza kufikia wastani asilimia 90 ya malengo ya muda Tanzania katika mwaka wa 2018 natunavo sherekea maka 6 ya fastjet Tanzania lengo letu nikutoa huduma kwa wakati ikiwa ni sehemu ya mikakati ya kuboresha huduma kwa Wateja kwa ujumla.’

Fastjet inaruka kati ya Dar es salaam na Mbeya, Kilimanjaro, Mwanza, Lusaka na Harare na ndege zenya ingini za jet. .
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: