Na Beberu Benjamin James.

Muziki mzuri na tungo bora ni mtetezi wa afya ya kisaikolojia na ya kimwili. Kusikiliza muziki mzuri na bora kunapunguza hisia, hupunguza unyogovu, na kuimarisha mfumo wa kinga, na kuboresha utendaji wa kimwili, hupunguza hisia ya uchovu na huongeza harakati za mwili na uratibu.

Muziki bora na tungo bora ni kama wimbo wa Kala Jeremiah feat Nuruwell Usikate Tamaa na wimbo mzuri ni mzuri ambao sio bora ni wimbo wa Rayvanny Ft Diamond Platnumz - Tetema .

Wimbo mwingine mzuri ni Alikiba – Kadogo na tungo maridhawa bora ni Fid Q Ft. Maua Sama, Hard Mad & Noorelly - Ulimi Mbili.

Siku zinavyozidi kwenda Tanzania tunapoteza kizazi cha wanamuziki makini wenye ubora na weredi katika uandishi na watizamani na wasikilizaji tumebariki video nzuri na kupumzisha masikio kupenda tungo nzuri .

Wasanii wamedhoofika kifikira katika uandishi, Interviews zao zimekuwa nyepesi sana na kuharibu ubora wa msanii kifikira.

Mtu mwingine hunyamaza kwani hana la kusema;na mwingine hunyamaza kwani anajua wakati wa kuongea ,tayarisha utakachosema nawe utasikilizwa; panga pamoja unayoyajua kisha ujibu .

Chidi Benzi , amejua wakati wa kuongea na mtu wa kuongea nae ,Chidi Benzi anapompa ushauri mkuu wa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda , na kuongea vitu vyenye tija ni jambo lililo nishtua sana.


Chidi Benzi,anaposema,’’mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam anatakiwa asimamie mambo yake ya msingi kama mkuu wa mkoa na kuachana na tabia ya kufuatilia kila jambo kama

1.Madawa ya kulevya yeye
2.Wasanii wa Bongo Flava yeye
3.Bongo Movies yeye
4.Wauza Cd yeye,anatakiwa afanye kitu kimoja mengine awaachie wengine,’’ maneno haya ni maneno yenye tija na umuhimu mkubwa kutoka kwa msanii ambaye ni kioo cha jamii.

Chidi Benzi ,ananipa sukari kwa ncha ya kisu ,nasikia utamu na uchngu kwa wakati mmoja ,nasikia utamu kwa maneno kama haya kutoka kwake sababu wanaojiita conscious mcees ni waoga kifikira wao hujikomba kwa viongozi badala ya kuwakanya viongozi ,nasikia uchungu kwa Chidi Benzi naposikia amerudi tena Rehab.

Mkuu wa mkoa anapowaita wasanii na kuwaambia ana bilion 2 ambazo anatakiwa wajadiliane jinsi ya kuzifanyia kazi na kuboresha kazi za wasanii lilikuwa ni jambo jema ila halikuwa wazo zuri ,sababu masuala yote ya michezo na burudani yapo chini ya Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dkt Mwakyembe.

Pesa haiwezi kukupa wazo bora ila wazo bora linaweza kukupa pesa bora,yatakiwa zitengenezwe sera na muundo wa usimamizi wa kazi za wasanii unaotambulika kikatiba na kisheria kwa manufaa ya wasanii wote walio hai na waliotangulia mbele za haki.

Wasanii wa siku hizi wapo karibu sana na viongozi wa serikali kuliko kuwa karibu na wananchi ,ni jambo la kawaida kuona msanii anashinda kwenye ofisi za viongozi wa serikali na kupiga picha na kupost kwenye mitandao ya kijamii na kuanza kumuandika mkuu wa mkoa .'' Baba Keagen,'' hakuna msanii aliyemtoa kasoro baba Keagen zaidi ya Chidi Benzi.

Chidi Benzi,ameongea ukweli mchungu na wenye tija ,wasanii wanatakiwa kubadili mtazamo wa fikira na kuanza kutunga nyimbo zenye tija katika maeneo yenye tatizo katika jamii kama ajira,malezi,ushoga,uhuru wa kujieleza na tatizo la malenzi ya mzazi mmoja.

Nani kasikiliza wimbo wa Nas - “Daughters” ?

Tanzania waandishi bora na maridhawa wa nyimbo zenye tija hawafiki wanne ,waliobaki ni mapenzi tu na uandishi mwepesi ,kazi kubwa ya msanii ni kukemea mabaya kukanya,kupongeza ni wakati wa kujitenga na wanasiasa na kuwa karibu na jamii.

Tambueni kuwa wanasiasa hawaingii kwenye show zenu ,wanasiasa wahanunui kazi zenu bali wanasiasa wanawatumi wasanii ,mnakumbuka Wimbo wa CCM Juma nature na Mangwair? Mangwair amekufa maskini wakati alikuwa na kipaji tatizo ni mfumo na sera za kusimamia michezo na burudani ni mibovu.

Najiuliza viongozi wanaokwenda Marekani kwa nini wasitengeneza vyombo vya kusimamia muziki kama 1.Broadcast Music, Inc. (BMI)
2.ASCAP-American Society of Composers, Authors and Publishers]
3.SESAC- Society of European Stage Authors and Composers
4. Pro Music Rights,
5.SoundExchange?

Kuna wasanii wengi ambao wanapewa promo kubwa ,lakini muda mwingi wanaonyesha mavazi na swagger ni wakati wa kubadili muundo na mfumo wa kuwapa promo na kuanza kuwatumia wasanii kama
1.Wabiro Noel Wassira Wakazi
2.Nikki Mbishi
3.One the Increidible sababu wana utundu wa fikira kuliko wale wasanii wanaopewa promo zaidi.

Chidi Benzi umeonyesha ukomavu, ujasiri na ubora wa mawazo kutoa kasoro bora sehemu inayosifiwa bila kukosolewa, Chidi Benz ametumia muda mwingi Rehab lakini yupo consious na wengine wapo huru ila mawazo yao na fikira zao zipo Rehab.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: