WAFANYAKAZI wa Ikulu Zanzibar na Ikulu Dar es Salaam wakifanya mazoezi ya viungo kabla ya kuaza kwa mchezo wa mpira katika Bonaza la Michezo ya Pasaka lililofanyika katika Uwanja wa Mao Zedung's. Zanzibar (Picha na Ikulu Zanzibar ).  
NAIBU Katibu Mkuu Ofisi ya Rais na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Ndg. Salum Kassim Ali akisalimiana na Wachezaji wa Timu ya Ikulu Sports Club Dar es Salaam, kabla ya kuaza kwa mchezo huo uliofanyika Uwanja wa Mao Zedung's Zanzibar.(Picha na Ikulu Zanzibar)
MCHEZAJI wa Timu ya Ikulu Sports Club Dar es Salaam Azori Ndege mwenye mpira akimpita beki wa Timu ya Ikulu Sports Clun Zanzibar Khamis Bakari wakati wa mchezo wao wa Bonaza la Pasaka uliofanyika katika Uwanja wa Mao Zedung's Zanzibar Timu ya Ikulu Zanzibar imeshinda bao 6-2.(Picha na Ikulu Zanzibar)
MSHAMBULIAJI wa Timu ya Ikulu Sports Club Zanzibar Rajab Wakil akimpita Beki wa Timu ya Ikulu Sports Club Dar es Salaam Okororo Sadiq, wakati wa mchezo wao wa Bonaza la Pasaka uliofanyika Uwanja wa Mao Zedung's Zanzibar Timu ya Ikulu Sports Club Zanzibar imeshinda mchezo huo kwa bao 6-2.(Picha na Ikulu Zanzibar)
MSHAMBULIAJI wa Timu ya Ikulu Sports Clun Zanzibar Omar Hamad akijaribu kumpita Beki wa Timu ya Ikulu Sports Club Dar es Salaam Hassan Econ, wakati wa mchezo wao wa kusherehekea Michezo ya Bonaza la Pasaka uliofanyika Uwanja wa Mao Zedung's Zanzibar Timu ya Ikulu Zanzibar imeshinda bao 6-2.(Picha na Ikulu Zanzibar)
MSHINDI wa mbio za Mita Mia Moja kutoka Ikulu Zanzibar Vuai Suleiman akiongoza mbio hizo na kufuatiwa mshindi wa Pili kutoka Ikulu Dar es Salaam Mwabora Richard (Picha Ikulu Zanzibar)
WASHIRIKI wa mchezo wa kufukuza Kuku kutoka Ikulu Zanzibar na Ikulu Dar es Salaam wakishiriki mbio hizo za kufukuza kuku mshindi kutoka Ikulu Zanzibar Bi. Susiati Nyange.(Picha na Ikulu Zanzibar)
WANAMICHEZO kutoka Timu ya Ikulu Sports Clun Dar es Salaam, wakisoma dua wakati walipotembelea Kaburi la Muasisi wa Mapinduzi ya Zanzibar na Rais wa Kwanza wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Mhe. Marehemu Mzee Abeid Amani Karume, katika viwanja vya Afisi Kuu ya CCM Kisiwangui Zanzibar, baada ya kumaliza mchezo wao leo.(Picha na Ikulu Zanzibar)
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: