Katibu wa Itikadi na Uenezi CCM mkoa wa Iringa Ramadhani Baraza akizungumza na waandishi wa habari katika ofisi za CCM Mkoa wa Iringa.
NA FREDY MGUNDA, IRINGA.

CHAMA cha mapinduzi (CCM) mkoa wa Iringa kimewataka wanachama na wadau wa chama hicho kuupuza ujumbe wa mbunge wa jimbo la Iringa mjini Peter Msigwa kuwa chama hicho kipo imara na sio dhaifu.

Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake Katibu wa Itikadi na Uenezi CCM mkoa wa Iringa Ramadhani Barazaalisema kuwa mbunge huyo anatakiwa kufanya mkutano wa hadhara kuwaaga wananchi wa mkoa wa Iringa kwa kuwa zama za kuiongoza manispaa ya Iringa umefika kikomo.

“Zama za Msigwa zimeisha kuongoza manispaa ya Iringa kwa kuwa wananchi wameshamchoka kwa kuwa sio kiongozi aliyewasaidia kuleta maendeleo kwani toka aingie madarakani hajawahi kufanya maendeleo yeyeto yale kwenye jimbo hili la Iringa” alisema Baraza

Baraza alisema kuwa chama cha mapinduzi kinasema hivyo kwa kuwa chama cha mapinduzi kipo imara kweli kutokana na aina ya uongozi walionao na mfumo wa siasa ambao wamekuwa wakiutumia kuwafikia wananchi wa mkoa wa Iringa.

“Saizi tumefanikiwa kuwafikia wananchi wa chini kabisa ambao kunakipindi huwa wanasaulika wakati ndio wapiga kura wetu hivyo tumerudi tumejipanga na tunaendelea kufikia kila siku kwa kupokea changamoto zao” alisema Baraza.

Lakini pia Baraza alisema kuwa wapinzani wamekuwa hawana jambo jipya ambalo wanaweza kuliteleza kwa kuwa serikali ya chama cha mapinduzi kimesimamia vilivyo serikali na kuhakikisha wanatatua changamoto za wananchi waliowapa mamlaka ya kuwaongoza.

“Wapinzani saizi kazi yao ni kueneza propaganda chafu ambazo sasa wananchi wamezichoka na hazina nafasi kwenye ulingo wa siasa safi na yakuleta maendeleo kwa wananchi” alisema Baraza

Baraza alisema kuwa chama cha mapinduzi sio dhaifu kwa kuwa kimefanikiwa kupata madiwani saba ambao wameamia kwenye chama cha mapinduzi kwa ajili ya udhaifu wa CHADEMA na viongozi wake wa mkoa wa Iringa.

“Moto wetu ndio kwanza umeanza hivyo tumwambie Msigwa ajipange kuondoka kwa kuwa saizi ameshakuwa dhaifu na hana jambo jipya ambalo linaweza kusaidia kuleta maendeleo kwa wananchi wa mkoa wa Iringa” alisema Baraza

Hoja hiyo imekuja siku kadhaa baada mbunge wa jimbo la Iringa kusema kuwa chama cha mapinduzi mkoa wa Iringa ni dhaifu na hakiwezi kumuondoa madarakani labda yeye aamue kung’atuka kwa hiyari yake.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: