Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli akishuhudia Mkuu wa Majeshi na Ulinzi Jenerali Venance Mabeyo akimbadilishia cheo kutoka Kanali hadi kuwa Brigedia Jenerali wa Jeshi la Wananchi Tanzania(JWTZ), Charles Mbuge wakati wa hafla ya uzinduzi wa Mji wa Serikali ulijengwa katika eneo la Mtumba jijini Dodoma leo. Brigedia Mbuge huyo amepewa cheo hicho na Mhe. Rais kufuatia uchapakazi wake katika kusimamia miradi ya ujenzi mbalimbali inayotekelezwa na Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ) kwa kushirikiana na JKT.
Rais na Amiri Jeshi Mkuu Dkt. John Pombe Magufuli, Makamu wa Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan, Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa na viongozi wengine wakishuhudia Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Jenerali Venance Mabeho akipokea saluti baada ya kumvisha cheo cha Brigedia Jenerali (aliyekuwa Kanali) Charles Mbuge baada ya kumpandisha cheo hicho kutokana na utendaji kazi wake katika kusimamia vyema ujenzi wa miradi mbalimbali ikiwemo ya ukutua wa Mererani, majengo ya ofisi za serikali na nyumba za watumishi wa umma jijini Dodoma. Hafla hii ya ghafla imefanyika wakati wa sherehe za uzinduzi wa mji wa Serikali eneo la Mtumba jijini Dodoma Jumamosi Aprili 13, 2019
Rais na Amiri Jeshi Mkuu Dkt. John Pombe Magufuli, Makamu wa Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan, Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa na viongozi wengine wakishuhudia Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Jenerali Venance Mabeho akimpongeza baada ya kumvisha cheo cha Brigedia Jenerali (aliyekuwa Kanali) Charles Mbuge baada ya kumpandisha cheo hicho kutokana na utendaji kazi wake katika kusimamia vyema ujenzi wa miradi mbalimbali ikiwemo ya ukutua wa Mererani, majengo ya ofisi za serikali na nyumba za watumishi wa umma jijini Dodoma. Hafla hii ya ghafla imefanyika wakati wa sherehe za uzinduzi wa mji wa Serikali eneo la Mtumba jijini Dodoma Jumamosi Aprili 13, 2019.
Rais na Amiri Jeshi Mkuu Dkt. John Pombe Magufuli akitangaza kumpandisha cheo cha Brigedia Jenerali (aliyekuwa Kanali) Charles Mbuge kutokana na utendaji kazi wake katika kusimamia vyema ujenzi wa miradi mbalimbali ikiwemo ya ukutua wa Mererani, majengo ya ofisi za serikali na nyumba za watumishi wa umma jijini Dodoma. Hafla hii ya ghafla imefanyika wakati wa sherehe za uzinduzi wa mji wa Serikali eneo la Mtumba jijini Dodoma Jumamosi Aprili 13, 2019.
Brigedia Jenerali (aliyekuwa Kanali) Charles Mbuge akipongezwa baada ya kumpandishwa cheo hicho na Rais Dkt. Magufuli kutokana na utendaji kazi wake katika kusimamia vyema ujenzi wa miradi mbalimbali ikiwemo ya ukutua wa Mererani, majengo ya ofisi za serikali na nyumba za watumishi wa umma jijini Dodoma. Hafla hii ya ghafla imefanyika wakati wa sherehe za uzinduzi wa mji wa Serikali eneo la Mtumba jijini Dodoma Jumamosi Aprili 13, 2019.
Brigedia Jenerali (aliyekuwa Kanali) Charles Mbuge akipongezwa na Mama Salma Kikwete baada ya kumpandishwa cheo hicho na Rais Dkt. Magufuli kutokana na utendaji kazi wake katika kusimamia vyema ujenzi wa miradi mbalimbali ikiwemo ya ukutua wa Mererani, majengo ya ofisi za serikali na nyumba za watumishi wa umma jijini Dodoma. Hafla hii ya ghafla imefanyika wakati wa sherehe za uzinduzi wa mji wa Serikali eneo la Mtumba jijini Dodoma Jumamosi Aprili 13, 2019
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: