Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Paul Makonda akimkabidhi gorikipa wa timu ya Simba kiasi cha shilingi milioni 10.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Paul Makonda akiwa katika picha ya pamoja na wachezaji wa timu ya Simba

Na Mwandishi Wetu.

Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Paul Makonda leo amewakabidhi wachezaji wa Simba kitita cha shilingi milioni 24 kama sehemu ya zawadi na hamasa kufuatia Timu hiyo kuchukuwa ubingwa wa Ligi kuu Tanzania bara na kuingia katika robo fainali ya Klabu bingwa Afrika.

RC Makonda amewataka wachezaji hao kutumia fedha hizo kuanzisha miradi ya maendeleo itakayowasaidia kujipatia  kipato pindi watakapostaafu mpira huku akiwataka kutumia umaarufu na Brand zao kujiingizia kutengeneza kipato.

Amesema katika mgawanyo wa fedha hizo Golikipa wa Simba Aish Manula amepokea kiasi cha Shilingi Milioni10, Wachezaji tisa Milioni 1 kila mmoja, Mchezaji bora wa kike wa Simba Queen Milioni 2 na Msemaji wa Simba Haji Manara ambae amepatiwa Milioni 3 kama sehemu ya kutambua mchango wake kwenye uhamasishaji wa mashabiki kujaa uwanjani.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: