NA K-VIS BLOG


WAZIRI wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dkt. Harrison Mwakyembe, ameongoza mamia ya waandishi wa habari na waombolezaji wengine kuaga mwili wa aliyekuwa Mhariri wa gazeti la Jamhuri, marehemu Godfrey Dilunga (43) kwenye viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam Septemba 19, 2019.

Viongozi wengine walioshiriki kwenye shughuli hiyo ni pamoja na Naibu Meya wa Manispaa ya Ilala, MMheshimiwa, Kumbilamoto, Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais Ikulu, Bw. Gerson Msigwa, Msemaji Mkuu wa Serikali na Mkurugenzi wa Idara ya Habari Maaelezo, Dkt. Hassan Abassi, Kiongozi wa ACT-Wazalendo na Mbunge wa Kigoma Mjini, Mhe. Zitto Kabwe na Waziri wa Mambo ya Nje na Uhusiano wa Kimataifa (Mstaafu), Mhe. Bernard Membe.

Wengine waliohudhuria ni pamoja na Katibu wa Halmashauri Kuu, Itikadi na Uenezi , CCM, Bw. Hamphrey Polepole, Mbunge wa Mtama, Mhe. Nape Nnauye, Mbunge wa Viti Maalum Mhe. Amina Mollel na Naibu Katibu Mkuu wa CHADEMA, Bw. Salum Mwalimu.

Aidha Wakuu wa vyombo mbalimbali vya habari nchini, wakiwemo waandishi wa habari walishiriki katika shughuli hiyo ya kumuaga marehem,u Dilunga aliuyefariki kwenye hospitali ya Taifa Muhimbili, wakati akipayiwa matibabu.

Kwa mujibu wa Mkurugenzi wa kampuni ya Jamhuri Media, inayochapisha gazeti hilo, Bw. Deodatus Balile, Dilunga alikuwa akisumbuliwa na maradhi ya Taifod pamoja na Malaria na aliaga dunia Septemba 17, 2019. Mwili wake umesafirishwa alasiri hii kuelekea alikozaliwa Mkoani Morogoro kwa mazishi.

Marehemu Dilunga ameacha mjane na watoto watatu.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: