Spika wa Bunge, Mhe. Job Ndugai (katikati) katika picha ya pamoja na Maspika wastaafu ambao ni Mhe. Anne Makinda (wa pili kushoto) na Mhe. Pius Msekwa (wa pili kulia) baada ya Sherehe fupi za kukabidhiana majoho kwa Maspika hao zilizofanyika leo Bungeni Jijini Dodoma. Kushoto ni Naibu Spika wa Bunge, Mhe. Dkt. Tulia Ackson na Mbunge wa Urambo, Mhe. Margaret Sitta.
Spika wa Bunge, Mhe. Job Ndugai (wa pili kulia) akimvalisha na kumkabidhi joho Mhe. Pius Msekwa alilokuwa akitumia wakati akiwa Spika wa Bunge la Nane Bungeni Jijini Dodoma. Kulia ni Katibu wa Bunge, Ndg. Stephen Kagaigai.
Spika wa Bunge, Mhe. Job Ndugai akimkabidhi joho Mhe. Margaret Sitta kwa niaba ya mume wake aliyekuwa Spika wa Bunge la 9 Mhe. Samuel Sitta wakati wa Sherehe fupi za kukabidhiana majoho kwa Maspika wastaafu zilizofanyika leo Bungeni Jijini Dodoma. Kulia ni Katibu wa Bunge, Ndg. Stephen Kagaigai.
Toa Maoni Yako:
0 comments: