
Hayo ameyasema wakati wa uzinduzi wa Jukwaa la Wazee wa Kata ya Mbwawa (JUWAKAM) ambapo amewataka kutumia jukwa hilo kujiimarisha kiuchumi na kuanzisha miradi endelevu.
Katika uzinduzi huo, Mstahiki Meya amekubali kuwa mlezi wa Jukwaa la Wazee Kata ya Mbwawa na kuwaahidi kuwa nao bega bega katika kubuni miradi yenye tija na hatosita kutafuta wadau wa maendeleo ili waweze kupata mtaji.
Dr Nicas amesema, kumekuwa na majukwaa mengi ya wazee yakianzishwa Kata tofauti ila JUWAKAM wana malengo mazuri hasa ukisikiliza risala yao ila changamoto kubwa inayokuja baadae ni uaminifu ndani ya majukwaa hayo.
![]() |
Amesema, majukwaa mengi yamekuwa yanadorora na miradi iliyopo kufa na kufikia hatua hadi kuuza vitu vya miradi ila anaamini JUWAKAM watakuwa wamejipanga kuweza kusimamia miradi hiyo ikiwemo kumtafuta msimamizi ambaye atakuwa anasimamia.Kwa upande wa Mwenyekiti wa JUWAKAM Bw. Sebastian Sanga amemshukuru Mstahiki Meya wa Manispaa ya Kibaha kwa kukubali kuwa mgeni rasmi kwenye uzinduzi wa jukwaa hilo pamoja na kukubali kuwa Mlezi wa JUWAKAM, jambo ambalo litaenda kuleta chachu ya kimaendeleo wa wazee wa Kata ya Mbwawa.
Amesema, Kata ya Mbwawa ina wazee 520 ambao wanatambulika na Jukwaa, na walianza mchakato wa kuanzisha jukwaa hili mwaka 2024 na hadi kufikia 2026 wamelisanili kwa mwongozo wa mabaraza ya Kata.





Toa Maoni Yako:
0 comments: