Meneja wa NMB Kanda ya Magharibi Leon Ngowi, akizungumza kwenye kikao cha wafanyabiashara ambao ni wateja wa benki hiyo na kusema lengo lake ni kujadili changamoto ambazo huwa zinawakabili wafanyabiashara ili kuboresha huduma kwao na kuendelea kuitumia benki kukopa fedha ili kuwainua kiuchumi - Picha zote na Marco Maduhu - Malunde1 blog.
Mwenyekiti wa wafanyabiashara Business Club wa Benki ya NMB Azan Salumu akiomba riba ipunguzwe ili wafanyabiashara wengi waweze kujitokeza kuchukua mikopo Benki, pamoja na kuweza kurejesha marejesho kwa wakati bila ya kukwama.
Mkuu wa wilaya ya Kahama Anamringi Macha akizungumza kwenye kikao hicho ambapo aliwataka wafanyabiashara wote wilayani humo kuacha tabia ya kukwepa kulipa kodi bali wajitokeze ili kuchangia ongezeko la mapato serikalini, fedha ambazo zitasaidia kuleta maendeleo wilayani humo ikiwamo na ujenzi wa miundombinu mizuri ya barabara ambayo itasaidia biashara zao kufanyika kwa ufanisi.
Afisa kutoka Mamlaka ya Mapato Tanzania TRA wilayani Kahama Deo Marisho akitoa elimu ya mlipa kodi na kubainisha kuwa kodi ndiyo chanzo kikubwa cha mapato serikalini na kuwataka pia pale wanapouza bidhaa zao watoe risiti.
Mtaalamu wa mafunzo kutoka EIB Fathili Boniphace akitoa elimu kwa wafanyabiashara hao namna ya kutumia fursa kupanua wigo wa biashara zao na hatimaye kukua kiuchumi.
Meneja wa benki ya NMB Tawi la Manonga mkoani Shinyanga Baraka Ladislaus akitoa salamu kwa wafanyabiashara wa wilaya ya Kahama ambao ni wateja wa benki hiyo wilayani humo.
Meneja wa Benki ya NMB kutoka Bukombe George Fundi akitoa salam kwa wafanyabiashara wa wilayani Kahama, ambao ni wateja wa benki hiyo.
Wafanyabiashara wa Kahama ambao ni wanachama wa Business Club tawi la Kahama wakiwa kwenye kikao chao na benki hiyo kwa ajili ya kujadili masuala mbalimbali yanayowahusu ikiwamo kupewa elimu ya mlipa kodi, namna ya kumudu marejesho ya mikopo,kupanua wigo wa biashara pamoja na kutatuliwa kero zinazowakabili hasa kupunguziwa riba ya mikopo.
Wafanyabiashara wakiendelea na kikao chao na wadau wao wa benki ya NMB Tawi la Kahama katika ukumbi wa Kapaya wilayani humo.
Mkuu wa wilaya ya Kahama Anamringi Macha akiwataka pia wafanyabiashara hao kuwa wanatunza kumbukumbu ya biashara zao.
Wafanyabiashara wakiendelea na kikao.
Kikao kikiendelea katika ukumbi wa Kapaya wilayani Kahama.
Meneja wa benki ya NMB Kanda ya Magharibi Leon Ngowi akielezea namna benki hiyo inavyowajali wateja wake ambapo imeweza kupunguza riba kwa wakopaji wa kati kutoka asilimia 21 mpaka 19, mikopo ya chini kutoka asilimia 23 mpaka 21, huku akiahidi kuendelea kutatua changamoto zingine ambazo zinawakabili wateja wao, ili waendelea kufurahia huduma katika benki hiyo.
Wafanyabiashara wakiendelea na kikao.
Kikao kikiendelea.
Kikao kikendelea kwa kusikiliza elimu mbalimbali kutoka kwa wataalamu ikiwamo ya mlipa kodi na namna ya kurejesha marejesho ya mikopo bila kukwama pamoja na kupanua wigo wa biashara kwa kutumia fursa
Viongozi wa Benki ya NMB, pamoja na mkuu wa wilaya Anamringi Macha wakipiga picha ya pamoja na wafanyabiashara washindi 15 kutoka Benki ya NMB tawi la Kahama.
Viongozi wa Benki ya NMB, pamoja na mkuu wa wilaya Anamringi Macha wakipiga picha ya pamoja na wafanyabiashara washindi 15 kutoka Benki ya NMB tawi la Kahama. Picha zote na Marco Maduhu- Malunde1 Blog.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: