Mchezo namba 72 wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara(TPL) kati ya Simba na Young Africans uliochezwa Jumapili Septemba 30,2018 Uwanja wa Taifa umeingiza mapato ya jumla ya shilingi milioni 404,549,000.

Mchezo huo ulioanza saa 11 jioni umeingiza jumla ya Watazamaji 50,168.

Mgawanyo wa mapato hayo ni kwenye upande wa VAT, Selcom, TFF, Uwanja, Simba, TPLB, gharama za mchezo, BMT na DRFA.

Kati ya fedha hizo VAT ambayo ni asilimia 18 ni shilingi milioni 61,710,864.41, Selcom milioni 17,901,293.25.

Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) milioni 16,246,842.12,Uwanja milioni 48,740,526.35.

Wenyeji wa mchezo Simba milioni 194,962,105.41, TPLB milioni 29,244,315.81, gharama ya mchezo 22,745,578.96, BMT milioni 3,249,368.42 na DRFA milioni 9,748,105.27
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: