Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Mhe. Christina Mndeme amemkabidhi Shilingi Milioni tano ndugu Benedict Mapunda kama zawadi ya kutambua jitihada alizofanya za kubaini moto uliokuwa unawaka Kwenye mgodi wa Makaa ya Mawe ya Luanda Mbinga mnamo 2006.

Mzee huyo alitoa taarifa kwa Mamlaka husika zilizowezesha kuzima moto huo na kuokoa rasilimali za Nchi.

Katika tukio hilo Mhe. Mndeme ameupongeza uongozi wa TANCOAL kwa kuendelea kumjali mzee huyo na kuamua kumuajiri katika mgodi huo wa Ngaka. Na Serikali itaendelea kutambua Mchango wake kwa Taifa.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: