Wachezaji na mashabiki wa timu ya mpira wa miguu ya Tanzania (Taifa Stars) watapelekwa nchini cape verde na ndege kubwa ya serikali ya boing 787 Dreamliner na kusubiliwa mpka siku ya kurudi.

Hayo yamesemwa na Waziri wa Habari Sanaa, Utamaduni na Michezo Dkt. Harrison Mwakyembe katika mkutano na waandishi wa habari uliofanyika mapema leo jijini Dar es Salaam.

Dkt. Mwakyembe alisema kuwa ndege hiyo ya Boing 787 Dreamliner itabeba wachezaji na mashabiki kwenda Cape Verde kwenye mchezo wa kuwania kufuzu fainali za mataifa ya Afrika hapo mwakani na kuwarudisha nchini kuwahi mchezo wa marudiano utakaopigwa Oktoba 16 kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.

kwa upande wa Shirikisho la Mchezo wa Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) linajitoa kilipia nafasi 31 huku nafasi zilizo baki ni za wadau na mashabiki watakaopenda kuipa nguvu timu ya taifa basi watalipia bei ya tiketi moja ni dola 1,500
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: