Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mhe. Ummy Ally Mwalimu ambaye alikuwa mgeni rasmi akizungumza na watoto na wageni waalikwa waliohudhuria katika sherehe ya siku ya watoto duniani iliyofanyika jijini Dar es Salaam.
Mratibu Mkazi wa Umoja wa Mataifa nchini Tanzania, Alvaro Rodriguez akizungumza katika maadhimisho ya siku ya watoto duniani iliyofanyika jijini Dar es Salaam.
Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Kimataifa la Kuhudumia Watoto (UNICEF) Bi. Maniza Zaman akizungumza  na watoto na wageni waalikwa waliohudhuria katika sherehe ya siku ya watoto duniani iliyofanyika jijini Dar es Salaam.

Wageni waalikwa wakifuatilia.
Mratibu Mkazi wa Umoja wa Mataifa nchini Tanzania, Alvaro Rodriguez akiteta jambo na mgeni mwalikwa.
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mhe. Ummy Ally Mwalimu ambaye alikuwa mgeni rasmi akisalimiana na Mratibu Mkazi wa Umoja wa Mataifa nchini Tanzania, Alvaro Rodriguez. 
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mhe. Ummy Ally Mwalimu ambaye alikuwa mgeni rasmi (kushoto) na Mratibu Mkazi wa Umoja wa Mataifa nchini Tanzania, Alvaro Rodriguez (kulia) wakifuatilia mijadala.
Miongoni mwa vijana waliotoa ushuhuda wao ni mtangazaji wa kituo cha radio Clouds FM, Millard Ayo (pichani), ambaye amesema yeye alisimamia ndoto yake hadi dakika ya mwisho licha ya vikwazo kadhaa alivyopambana navyo.
Miongoni mwa vijana waliotoa ushuhuda wao ni aliyewahi kuwa Miss Tanzania 2012 Briggitte Alfred Lyimo (pichani), ambaye kwa sasa anajishughulisha na kusaidia watuu wenye ulemavu wa ngozi.
Mwenyekiti wa Baraza la Watoto la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, mtoto Joel Festo akitoa shukrani zake za pekee kwa wageni walioweza kufika katika sherehe yao.

SHIRIKA la Kuhudumia Watoto Duniani (Ofisi ya Tanzania), leo Novemba 27, 2018 imeungana na watoto wote duniani kusherehekea siku ya kimataifa ya watoto iliyofanyika jijini Dar es Salaam.

Hafla hiyo ambayo mheni rasmi alikuwa Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, wazee na watoto, Mhe. Ummy Mwalimu, ilishuhudia mamia ya watoto wakisikiliza ushuhuda kutoka kwa watoto na vijana ambao walieleza namna ya kusimamia ndoto aliyonayo my ili kuifikia.

Miongoni mwa vijana waliotoa ushuhuda wao ni mtangazaji wa kituo cha radio Clouds FM, Millard Ayo, ambaye amesema yeye alisimamia ndoto yake hadi dakika ya mwisho licha ya vikwazo kadhaa alivyopambana navyo.

Amesema darasani hakuwa "mzuri" sana, na hivyo hakuwa na hamu ya kuendelea na masomo kwani hakuwa akifanya vizuri, lakini kichwani mwake alikuwa na ndoto ya kuwa mtangazaji siku moja.

Millard Ayo ambaye pia ni mmiliki wa mtandao wa kijamii wa Millard Ayo.com, amesema, jitihada zake za kufikia ndoto hiyo zilitimia lakini jambo la muhimu ambalo amewaasa watoto kulizingatia ni kutokuwa na tamaa, na kufanya kazi kwa bidi na kwa uaminifu na kumtanguliza Mungu mbele.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: