Boharia Mkuu Crepin Bulamu akisoma taarifa kwa Waziri wa Maji na Umwagiliaji Profesa Makame Mbarawa wakati alipotembelea bohari ya maji (Maji Central Stores) kwa ajili ya kufahamu mambo mbalimbali.
Waziri wa Maji na Umwagiliaji Profesa Makame Mbarawa akieleza jambo kwa Boharia Mkuu Crepin Bulamu baada ya kutembelea ghala la vifaa na madawa leo Jijini Dar es Salaam.

Waziri wa Maji na Umwagiliaji Profesa Makame Mbarawa akikagua baadhi ya vifaa vilivyopo ndani ya ghala ndani ya bohari kuu ya maji Jijini Dar es Salaam.
Vifaa mbalimbali vilivyopo ndani ya Bohari kuu ya maji ambapo vina muda mrefu bila kutumika.

Na Cathbert Kajuna - Kajunason/MMG.

WAZIRI wa Maji na Umwagiliaji Profesa Makame Mbarawa amesema lengo la serikali ni kuona bohari kuu ya maji inasaidia katika kupunguza gharama za madawa.

Ameyasema hayo baada ya kutembelea bohari kuu ya maji (Maji Central Stores) na kusisitiza uongozi uliopo hauridhishi kutokana na namna wanavyoendesha taasisi hiyo.

Akizungumza na waandishi wa habari, Prof Mbarawa amesema nia ya serikali ni kuona mamlaka zinafaidika na bohari kuu na muda mwingine wanatakiwa kusambaza vifaa vyake kwa mamlaka za maji kote nchini.

Mbarawa amesema, kuna mita zaidi ya 10,000 zimefungiwa tu ndani hawazisambazi kwa mamlaka za maji, kuna miradi mingi imesimama kutokana na kukosa vifaa ila bohari kuu imeviweka na havifanyi kazi yoyote.

Amewaagiza bohari kuu ndani ya wiki mbili wawe wamesambaza mita hizo kwa mamlaka za maji nchini ikiwemo Mkoa wa Lindi ambao wana uhitaji wa mita za maji karibia 3,000 na mikoa mingine pia.

"Mimi hii ni mara yangu ya kwanza kufika hapa na nilikuja ili niweze kufahamu na kujifunza namna bohari kuu inavyofanya kazi ila nimefika hapa nimekuta vifaa vingi sana ambavyo vinahitajika kwenye miradi inayoendelea na mingine imesimama na hili suala linaonesha utendaji wa watu hawa hauko makini na hauridhishi,"amesema Mbarawa.

"Lengo ni kuona bohari kuu ni kujipanga katika upande wa madawa na bohari wanatakiwa kuuza madawa kwa mamlaka na wao wakinunua kutoka kiwandani kabisa na sio kwa watu au makampuni," amesema.

Naye Boharia Mkuu Crepin Bulamu amesema, ni kweli kuna vifaa vipo hapo ila sio kama havina ubora ila atafanya maagizo kama aliyooelekezwa na Waziri husika ya kuanza kusambaza vifaa hivyo kwa mamlaka za maji nchini.\

Bilamu ameagizwa kuteketeza dawa zote zilizoisha muda wake zisije kwenda kwa mamlaka kwa ajili ya matumizi ambao yanaweza kuleta athari kwa binadamu.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: