Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Ajira na Vijana Anthony Mavunde (wa pili kushoto), Mkurugenzi Mtendaji wa benki ya UBA Tanzania Limited Usman Isiaka (wa tatu kulia) wakiwa kwenye picha ya pamoja na baadhi ya wajasiriamali 48 kutoka Tanzania ambao wamefaidika na Dola 10,000 kila mmoja zilizotolewa na Tony Elumelu kwa ajili ya kuendeleza biashara. Taasisi ya Tony Elumelu imewekeza vya kutosha kwa wajasiriamali wa Tanzania ambao jumla yao waliofanikiwa ni 114 tangu 2015 na hivyo thamani ya jumla ya Dola za Marekani 1,140,000 zimetumika kupitia na programu za maendeleo.

Wajasiriamali 48 kutoka nchini Tanzania wamepatiwa dola 10,000 kutoka kwa Taasisi ya Tony Elumelu kwa kushirikiana na benki ya UBA Tanzania.

Akizungumza jijini Dar es Salaam wakati wakutangaza wajasiriamali hao ambao wamejishindia kiasi hicho kutokana na ubunifu wao wa kibiashara, Mkurugenzi Mtendaji wa benki ya UBA Tanzania Usman Isiaka alisema kuwa maono ya Taasisi ya Tony Elumelu (TEF) ni kuondoa vikwazo ambavyo wajasiriamali kutoka Afrka wanapitia wakijitahidi kuinua biashara zao kutoka kuwa ndogo hadi makampuni makubwa kitaifa na kimataifa.

Alisema hatua hiyo ni maono ya mwanzilishi wa makampuni ya Heirs Holding kutoka Nigeria, ambapo pia ni mwanzilishi wa Taasisi ya Tony Elumelu Foundation na Mwanyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa United Bank of Afrika (UBA) ambayo inafanya biashara kwenye nchi 20 Barani Afrika.

Isiaka alisema kuwa katika miaka saba tangu Taasisi kuanzishwa, TEF ilichukua muda kutafakari kasi ya taasisi za ndani na kuanza kubadilisha hadithi kimataifa na kuhamasisha ujasiriamali wa Afrika.

Mwaka 2015, TEF iliimarisha mipango na malengo na kufanya wajasiriamali na viongozi wa biashara kuchanua Afrika kama kituo kikubwa kijacho cha kuwekeza, aliongeza Isiaka.

TEF ilitaka kubadili ajenda ili maendeleo ya uchumi yasiwe tena kuhusu msaada wa kigeni. Tunaonyesha mabadiliko ya Afrika yanapaswa kusukumwa na Waafrika wenyewe.

Hii inaendana na sera ya sasa ya Serikali ya Tanzania kujiimarisha kiuchumi na viwanda. Tanzania peke yake, imewekeza vya kutosha kwa wajasiriamali ambao jumla yao waliofanikiwa ni 114 tangu 2015 na hivyo thamani ya jumla ya Dola za Marekani 1,140,000 zimetumika kupitia na programu za maendeleo.

Mwaka 2018, Watanzania walionufaika kupitia programu ya TEF ambapo jumla ya Dola za Marekani 480,000 kutoka Dola 170,000 mwaka 2015 zilitumika, alisema Isiaka.

Kwa upande wake, Mgeni Rasmi katika hafla hiyo, Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Ajira na Vijana Anthony Mavunde alisema anaona fahari kuwa kwenye hafla hiyo iliyoandaliwa na benki ya United Bank of Africa (Tanzania) Limited kwa ajili ya Taasisi ya Tony Elumelu 2018 ambayo iko chini ya Mwenyekiti wa Makampuni ya UBA Plc Nigeria, Tony Elumelu na ijajihusisha na majukumu ya kijamii.

Naelewa kwa heshima kubwa kwamba maono ya Taasisi ya Tony Elumelu (TEF) ni kufungua vikwazo ambavyo wajasiriamali kutoka Afrika wanapitia kuinua biashara zao kutoka kuwa ndogo na za kati (SMEs) hadi makumpuni makubwa ya kitaifa na kimataifa, Mavunde alisema.

Taasisi hiyo iliyoanzishwa 2010, imeanzisha mipango mbali mbali ambayo imeanza kubadili hadithi duniani kote kuhusu mchakato wa maendeleo ya kiuchumi wa kijamii nchini Afrika kupitia mtazamo maalumu juu ya majukumu ya wajasiriamali wadogo wenye mamlaka katika nchi za Kiafrika.

Taasisi ya Tony Elumelu imedhamiria kuwasaidia wajasiriamali kutoka Afrika kupitia Programu ya Taasisi ya Tony Elumelu ambayo inatoa mafunzo, ushauri na mtaji kuanzia kwa vijana wateule wa Afrika ambao wana Mawazo mazuri ya kibiashara. Kila kijana anapewa msaada wa fedha wenye dhamani ya Dola za Marekani 10,000 ambapo Dola 5,000 ni fedha taslimu.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: