Waziri wa Maji na Umwagiliaji Profesa Makame Mbarawa akizungumza na wananchi wa eneo la Mtoni Mashine ya maji na kuwataka kutunza vyanzo vya maji ili viwe endelevu na kuacha kulima pembezoni mwa mito. Picha zote na Cathbert Kajuna - Kajunason/MMG.
Wananchi wakimsikiliza Waziri Mbarawa.
Waziri akiagaa na wananchi.
Mti Kizinga ambao ni chanzo cha maji. 
Msafara eneo la tukio katika upandaji miti.
Waziri wa Maji na Umwagiliaji Profesa Makame Mbarawa akipanda mti kwenye Chanzo cha Mto Kizinga ikiwa ni kampeni ya Upandaji miti pembenzoni mwa vyanzo vya maji.
Mkuu wa Wilaya ya Temeke Felix Lyaniva akiwa anapamba mti kwenye Chanzo cha Mto Kizinga ikiwa ni kampeni ya Upandaji miti pembenzoni mwa vyanzo vya maji.
Afisa Mtendaji Mkuu wa Mamlaka ya Majisafi na Majitaka Dar es Salaam ( DAWASA) Mhandisi Cyprian Luhemeja akipanda mti kwenye Chanzo cha Mto Kizinga ikiwa ni kampeni ya Upandaji miti pembenzoni mwa vyanzo vya maji
Waziri wa Maji na Umwagiliaji Profesa Makame Mbarawa akizungumza na wanahabari mara baada ya kumaliza zoezi la kupanda miti.

Na Cathbert Kajuna - Kajunaso/MMG.

WAZIRI wa Maji na Umwagiliaji Profesa Makame Mbarawa amewaomba wananchi kutunza vyanzo vya maji ili viwe endelevu na kuacha kulima pembezoni mwa mito.

Ameyasema hayo leo wakati wa upandaji miti aina ya Mitomondo pembezoni mwa mto Kizinga akiwa ameambatana na Mkuu wa Wilaya ya Temeke Felix Lyaniva na Afisa Mtendaji Mkuu wa Mamlaka ya Majisafi na Majitaka (DAWASA) Mhandisi Cyprian Luhemeja.

Akizungumza na wananchi wa eneo la Mtoni Mashine ya maji, Profesa Mbarawa amesema wananchi wanatakiwa kulinda vyanzo vya maji ili wapate majisafi na salama kwa manufaa yaona vizazi vijavyo.

Amesema, amehakikisha wanaanza kampeni maalumu kwa ajili ya kulinda vyanzo vya maji, na wakivilinda vizazi vijavyo vitapata maji safi na salama na serikali watapoteza pesa nyingi iwapo wananchi wataharibu vyanzo hivyo.

Amesema Serikali inatumia pesa nyingi kujenva miundo mbinu ya maji na iwapo vyanzo vikiharibikiwa na basi haitaweza kufanya kazi ya kusambaza maji safi na salama.

"Lazima tusimamie sheria, serikali inawekeza hela nyingi sana katika kujenga miundo mbinu na kampeni hii imeanzia Mtwara, Ruvuma na Dar es salaam na hii itaendelea nchi nzima,"amesema Mbarawa.

Mkuu wa Wilaya ya Temeke Felix Lyaniva amesema mtambo huu wa maji wa Mtoni ulijengwa mwaka 1949 ukihudumia mkoa mzima wa Dar es Salaam.

Lyaniva amewasihi wananchi wanaoishi pembezoni mwa mto Mzinga kuacha kulima kwani kufanya hivyo wanasababisha maji kukauka na kusababisha ukosefu wa maji.

"Nilianza na nitaendelea kupanda miti pembezoni mwa vyanzo vya maji, suala hili nimeliwekea kipaumbele kwani maji ni muhimu na wananchi wanahitaji maji," amesema Lyaniva.

Naye Afisa Mtendaji Mkuu wa DAWASA Cyprian Luhemeja amesema kuna changamoto kubwa ya uharibifu wa vyanzo vya maji kwa wananchi kulima pembezoni mwa mto na wameanza kampeni hii ya kupanda miti kwenye maeneo yote.

Luhemeja amesema, wameanza kupanda miti katika chanzo cha mto Kizinga na watafuata kwenye mto Ruvu ili kulinda vyanzo hivyo kwa kupanda miti ya mitomondo inayoweza kuhimili ukame kwa muda mrefu.

Miti takribani 10,000 itapandwa kwenye chanzo cha mto Kizinga kwa kipindi tofauti na Desemba 9 mwaka huu watashirikiana na wananchi wapenda maendeleo na wafanyakazi wa DAWASA kupanda pindi kwenye chanzo cha mto Ruvu.

Chanzo cha mto Kizinga kinazalisha maji lita Milioni tisa kwa siku maji yanayosambazwa kwenye maeneo ya Mtoni, Kurasini, Mtoni Kijichi na Chang'ombe.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: