Baadhi ya madereva wa Uber wakibadilishana mawazo eneo la Ubungo Business Park muda mfupi kabla ya kuanza msafara ambao ulizunguka sehemu mbali mbali za jijini la Dar es Salaam kwa ajili ya kutangaza ushirikika kati ya Tigo na Uber ambapo mteja akilipa kwa Tigo Pesa anapata punguzo.
 Baadhi ya Madera wa Uber wakitoka kwenye magari yao muda mfupi baada msafara wao uliokuwa na magari 50 kwasili katika kituo cha Daladala Mawasiliano jijini Dar es Salaam. Wasafiri watakaotumia Uber katika kipindi cha Fiesta na kulipa kwa Tigo Pesa watapata punguzo la bei.
 Baadhi ya wananchi katika kituo cha Daladala Mawasiliano jijini Dar es Salaam wakiyatizama magari ya Uber yaliyosimama kituoni hapo yakipita sehemu mbali mbali za jijini kuhamasisha matumizi ya usafiri wa uhakika na gharama nafuu wa Uber ambapo watumia watakaotumia katika kipindi hiki cha Tigo Fiesta na kulipa kwa Tigo Pesa watapata punguzo.
 TUNAWEZA: Baadhi ya akina dada ambao ni madereva wa usafiri wa teksi wa Uber wakiwa katika picha ya pamoja wakati msafara wa magari hayo ulipozuru mitaa mbali mbali ya jiji la Dar es Salaam kuhamasisha matumizi ya usafiri huo wa uhakika, salama na kwa bei nafuu huku wateja wakifurahia punguzo la gharama ya usafiri huo wanapolipa kwa Tigo Pesa. 
Msafara wa magari ya Uber ukiwa katika eneo la Ubungo jijini Dar es Salaam ukielekea eneo la Mawasiliano kuhamasisha matumizi ya usafiri huo wa uhakika, salama na kwa bei nafuu. Watumiaji wa Uber watapata punguzo la bei katika msimu huu wa Tigo Fiesta watakapolipa usafiri huo kwa Tigo Pesa.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: