*Mahakama yaagiza fedha zake Milioni 90/- arudishiwe
*Ushahidi wa upande wa mashtaka ulikuwa umejaa hisia

Na Ripota Wetu, Globu ya jamii

MKURUGENZI wa Kampuni ya Kiluwa Steal Group. Co.ltd na Kiluwa Free Processing Zone Mohamed Kiluwa (50) aliyekuwa akikabiliwa na shtaka la kutoa rushwa ya Sh.milioni 90 kwa Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi ameshinda kesi baada ya upande wa mashtaka
kushindwa kuthibitisha mashtaka dhidi yake.

Hivyo Mahakama ya Wilaya ya Ilala jijini Dar es Salaam leo Desemba 24,2018 imemuchia imeamuru Kiluwa ambaye pia ni mfanyabiashara na kuagiza arudishuwe fedha zake Sh.milioni 90 anazodaiwa kutaka kutoa rushwa kwa Waziri Lukuvi.

Hukumu  ya kesi hiyo imetolewa na hiyo Hakimu Mkazi wa Mahakama hiyo, Samweli Obas ambapo amesema katika kifungu cha sheria namba 15(1)B(2) Cha Sheria  ya Kuzuia na Kupambana na rushwa ili mtu atiwe hatiani lazima vitu viwili vithibitike ikiwemo nia ovu ya kutoa fedha na kutoa fedha hizo ili
afanye au aache kufanya  jambo fulani.

Pia amesema katika mashahidi wa upande wa mashitaka, Shahidi wa watu watano na vielelezo saba vilivyowalishwa mahakamani hapo  vilikuwa vya hisia, hivyo Mahakama haiwezi kumtia hatiani mshitakiwa kwa ushahidi huo.Amefafanua ushahidi wote wa upande wa mashitaka umekaa kihisia, mlalamikaji alikuwa anahisi kupewa rushwa, hivyo hata kama hisia inanguvu kiasi gani Mahakama haiwezi kumtia hatiani mshitakiwa kwa hisia tu.

 "Katika ushahidi wao,  upande wa mashtaka ulidai kuwa kwa nia ovu mshtakiwa alimpatia Waziri kiasi hicho cha fedha, , hivyo miongoni mwa maswali aliyojiuliza ni kama mshtakiwa alikuwa na nia ovu ya kumpatia Waziri fedha hizo kama kishawishi ama zawadi au malipo ya kufanya jambo fulani,"amesema.

Aidha alijiuliza swali jingine kuwa ni kweli mshtakiwa alitoa fedha hizo kwa Waziri kwa sababu akiachia mlalamikaji mashahidi wengine wa upande wa mashitaka walitoa ushahidi wao walioambiwa na mlalamikaji au kusikiliza audio CD iliyowasilishwa mahakamani hapo.

Amesema ukiondoa mashahidi wote, ushahidi wa msingi ni wa mlalamikaji mwenyewe ambao ni lazima uchukuliwe kwa tahadhari lakini katika ushahidi wake mlalamikaji aliieleza mahakama kuwa hati za Kiluwa zimepatikana kihalali, hivyo anakiri zilitolewa kihalali. Ameongeza  pia msiri wake alimwambia mshtakiwa atamletea Dola za Marekani 50,000  ila zilizokamatwa ni Dola 40,000, hivyo Mahakama ina
mashaka.

Hakimu Obasi ameongeza kielelezo cha CD kina mashaka kwa sababu kina mapungufu ambapo ukiisikiliza mwanzo hadi mwisho wa CD hakuna kauli ambayo ameitoa mshtakiwa akisema anatoa Dola 40,000 pia katika CD hiyo ilisikika sauti ya mshitakiwa akisema "Ninachokifanya kama ndugu sitoi hongo wala nini nakupatia hichi kidogo kama mafuta ila sitoi hongo kama nakwenda tofauti mimi ni ndugu yako niambie,"

Hakimu alisema katika maneno hayo na kwamba Hakuna mahali ambapo mshitakiwa alisema anatoa hongo au anampatia Waziri dola 40,000 hivyo maelezo  hayo ya CD hayatoshelezi kusema alikuwa anatoa rushwa.
Hakimu Obasi akiendelea kusoma Hukumu hiyo kwa kuuchambua  uliowasilishwa mahakamani hapo Amesema, kilichopelekwa mahakamani hapo ni CD na si kifaa kilichorekodi hivyo mahakama hawezi
kujiridhisha kuwa sauti iliyopo kwenye CD hiyo ndio ya mshitakiwa.

Kwa mantiki hiyo basi, ushahidi uliotolewa na upande wa mashtaka haukuitosheleza mahakama na kuweza kumtia hatiani mshtakiwa, hivyo Mahakama inamuachia huru na fedha alizokuwa nazo Milioni 90 arudishiwe.


Mahakama ya Wilaya ya Ilala jijini Dar es Salaam leo Desemba 24,2018 imemuachia huru mfanyabiashara Mohamed Kiluwa (50)  (Pichani kushoto) ambaye ni Mkurugenzi wa Kampuni ya Kiluwa Steal Group. Co.ltd na Kiluwa Free Processing Zone aliyekuwa akikabiliwa na shtaka la kutoa rushwa ya Sh. Milioni 90 kwa Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi baaada ya upande wa mashtaka kushindwa kuthibitisha shtaka hilo la rushwa dhidi yake.
Mfanyabiashara Mohamed Kiluwa (50)  (Pichani kulia)  ambaye ni Mkurugenzi wa Kampuni ya Kiluwa Steal Group. Co.ltd na Kiluwa Free Processing Zone akiwa na Wakili wake Imani Madega wakitoka Mahakama ya Wilaya ya Ilala jijini Dar es Salaam baada ya kuachiwa huru katika kesi iliyokuwa ikimkabili ya kudaiwa kutoa rushwa ya Sh. Milioni 90 kwa Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi,ambapo upande wa mashtaka umeshindwa kuthibitisha shtaka hilo la rushwa dhidi yake.
 Mfanyabiashara Mohamed Kiluwa (50) akiwa na Mkewe wakipeana mikono kutoka kwa ndugu na jamaa,mara baada ya kutoka Mahakama ya Wilaya ya Ilala jijini Dar es Salaam baada ya kuachiwa huru katika kesi iliyokuwa ikimkabili ya kudaiwa kutoa rushwa ya Sh. Milioni 90 kwa Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi,ambapo upande wa mashtaka umeshindwa kuthibitisha shtaka hilo la rushwa dhidi yake.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: