Mmoja wa washindi wa zawadi ya kilaa siku ya shilingi milioni moja kwenye promosheni ya Jigiftishe inayoendeshwa na kampuni ya Tigo, Asha Shaban (wa pil kulia) akipokea mfano wa hundi kutoka kwa Meneja Bidhaa waa Tigo, Suleiman Bushangama (kushoto) pamoja na Jafary Othman - Mtaalam wa Huduma za Tigo (wa pili kushoto) katika hafla fupi ya kuwakabidhi washindi zawadi zao iliyofanyika eneo la Tabata jijini Dar es Salaam. Wa kwanza kulia ni Balozi wa promosheni hiyo, mtangazaji Mina Ally.
Mmoja wa washindi wa zawadi kila siku ya shilingi milioni moja kwenye promosheni ya Jigiftishe inayoendeshwa na kampuni ya Tigo, Anna Eliudi Makala (wa pili kulia) akipokea mfano wa hundi kutoka kwa Meneja Bidhaa wa Tigo, Suleiman Bushangama (kulia) pamoja na Jafary Othman - Mtaalam wa Huduma za Tigo (wa pili kulia) katika hafla fupi ya kuwakabidhi washindi zawadi iliyofanyika Tabata jijini Dar es Salaam.
Mshindi wa zawadi ya wiki ya shilingi milioni 10 katika promosheni ya Jigiftishe inayoendeshwa na kampuni ya Tigo, Iyaka Seifu Muinga (kulia) akipokea mfano wa hundi kutoka kwa Meneja Bidhaa wa Tigo, Suleiman Bushangama (kulia) pamoja na Jafary Othman - Mtaalam wa Huduma za Tigo (wa pili kulia) katika hafla fupi ya kumkabidhi washindi zawadi eneo la Tabata jijini Dar es Salaam. Wa pili kulia ni Balozi wa promosheni hiyo, mtangazaji Mina Ally.
Mshindi wa zawadi ya wiki ya shilingi milioni 10 katika promosheni ya Jigiftishe na Tigo, Iyaka Seifu Muinga (wa nne kulia) akiwa katika picha ya pamoja na washindi wengine wa kila siku wa
Mmoja wa washindi wa zawadi ya kila siku ya shilingi milioni moja katika promosheni ya Jigiftishe inayoendeshwa na kampuni ya Tigo, Idrisa Selemani (kulia) akipokea mfano wa hundi kutoka kwa Meneja Bidhaa wa Tigo, Suleiman Bushangama (kushoto) pamoja na Jafary Othman - Mtaalam wa Huduma za Tigo (wa pili kushoto) katika hafla fupi ya kuwakabidhi washindi zawadi eneo la Tabata jijini Dar es Salaam. Wa pili kulia ni Balozi wa promosheni hiyo, mtangazaji Mina Ally.

Na Mwandishi Wetu

Kitita cha shilingi milioni 10 cha mshindi wa kila wiki katika promosheni inayoendelea ya Tigo Jigiftishe, kimenyakuliwa na Iyaka Seifu Muinga, anayefanya kazi ya kuosha magari Tabata jijini Dar es Salaam.

Muinga anakuwa ni mshindi wa pili wa zawadi ya shilingi milioni 10 baada ya milioni kumi ya kwanza kuchukuliwa na David John Mmuni mkazi wa Changanyikeni jijini Dar es Salaam.

Akipokea zawadi yake katika eneo analofanyia kazi kutoka kwa Meneja wa Biashara wa Tigo, Suleiman Bushangama, mshindi huyo alielezea furaha yake na ksema kuwa Tigo imemkomboa kwa kuwa amepata mtaj wa kufungua biashara.

‘Nimefurahi sana kuibuka na mtaji huu kutoka promosheni ya Jigiftishe. Nitatumia pesa hizi kufungua biashara, ila kusema kweli sina mpango wa kuacha kazi yangu ya sasa,” Iyaka alisema huku akishangiliwa na wafanyakazi wenzake waliomsindikiza jukwaani kupokea zawadi.

Akiongea wakati akimkabidhi mshindi huyo zawadi yahe, Bushangama aliwataka wateja kuendelea kutumia huduma mbali mbali za Tigo ili kujishindia mamilioni ya shilingi yaliyotengwa kwa ajili ya kuwazawadia katika msimu huu wa sikukuu

Pamoja na kukabidhi zawadi ya shilingi milioni kumi kwa mshindi wa wiki, washindi wengine kumi wa kila siku kutoka mkoa wa Dar es Salaam walizawadiwa shilingi milioni moja kila mmoja.

Promosheni hiyo ya Jigiftishe inayoendeshwa na kampuni ya Tigo inalenga kuwazawadia wateja wanaotumia huduma za mtandao huo katika kipindi hiki cha sikukuu na mwaka mpya.

Jigiftishe inalenga kuongeza idadi ya mamilionea katika mzimu huu wa sikukuu kwa kutoa zawadi kumi za shilingi milioni moja kila siku, zawadi moja ya shilingi milioni kumi kila wiki na zawadi kwa washindi wa jumla za shilingi milioni 15, milioni 25 na milioni 50 itakayotolewa mwisho wa promosheni hiyo inayoendelea.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: