* Asema kustaafu sio dhambi bali ni heshima kwa Taifa
* Asisitiza hakuna sababu ya kuwasumbua wastaafu

Na Said Mwishehe,Globu ya Jamii

RAIS Dk.John Magufuli amerejesha matumaini mapya kwa wafanyakazi na kuagiza wastaafu wote nchini walipwe kwa kutumia kikotoo cha zamani cha asilimia 50.
Pamoja na hilo amesema kuwa kustaafu si dhambi bali ni heshima kwa Taifa.
Ametoa uamuzi huo leo hii Desemba 28, mwaka 2018 katika kikao chake kilichohudhuriwa na wadau wote wa mifuko ya hifadhi ya jamii ,wafanyakazi na viongozi wa ngazi mbalimbali wa mifuko hiyo.

Baada ya Rais kutangaza kutumika kwa kikotoo cha zamani ukumbi wa Ikulu uligeuka kuwa sehemu ya shangwe ambapo nyimbo za mshikamano kwa wafanyakazi zilianza kuimbwa huku Rais akiwaambia "Wafanyakazi Hoyee...wafanyakazi ni muhimu katika kipindi hiki na lazima wapewe stahiki zao na fomuka nzuri ni ile ya kuboresha maslahi ya watu na sio kuwa na fomula inayotesa wafanyakazi."

Akifafanua wakati anatoa uamuzi huo Rais Mafuli amesema kwamba "kustaafu si dhambi bali ni jambo la heshima. Anayestaafu anastahili kuheshimiwa na Taifa hili na hivyo hatakiwi kupata shida , kikokotoo kilichokuwa kinatumika huko nyuma kitumike katika kipindi hiki cha mpito hadi mwaka 2023," amesema Rais huku akishangiliwa.

Amefafanua kuwa kwa takwimu alizonazo ni kwamba kwa kipindi cha mpito ambacho ni kuanzia sasa hadi mwaka 2023 watakaostaafu ni wanachama 58, 000 na hao walipwe kwa kikotoo cha asilimia 50 huku akisisitiza mifuko yote ilipe kama ilivyokuwa inalipa awali.

Ameongeza kuwa Serikali iliyopo madarakani imeweka mfumo imara wa ukusanyaji kodi na miongoni mwa walipa kodi wazuri ni wafanyakazi na hivyo lazima waendelee kulipwa kama zamani ndani ya kipindi hicho cha mpito.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa meza kuu na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi na Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Kazi, Vijana, ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Jenista Mhagama na viongozi wa wafanyakazi na wa mifuko ya hifadhi ya jamii wakiwa wameshikana mikono kwa furaha huku wakiimba wimbo wa hamasa wa mshikamao wa wafanyakazi wa "Solidarity Forever" baada ya kuwasikiliza hoja zao, kuwahutubia na hatimaye kulipatia jawabu swala la vikokotoo vya wafanyakazi alipokutana nao Ikulu jijini Dar es Salaam leo Ijumaa Desemba 28, 2018.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa meza kuu na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi na Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Kazi, Vijana, ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Jenista Mhagama alipoongea na viongozi wa wafanyakazi na wa mifuko ya hifadhi ya jamii  baada ya kuwasikiliza hoja zao, kuwahutubia na hatimaye kulipatia jawabu swala la vikokotoo vya wafanyakazi alipokutana nao Ikulu jijini Dar es Salaam leo Ijumaa Desemba 28, 2018
 Viongozi wa wafanyakazi na wa mifujo ya hifadhi ya jamii wakiwa na furaha huku wakiimba wimbo wa hamasa wa mshikamao wa wafanyakazi wa "Solidarity Forever" baada ya kuwasikiliza hoja zao, kuwahutubia na hatimaye kulipatia jawabu swala la vikokotoo vya wafanyakazi alipokutana nao Ikulu jijini Dar es Salaam leo Ijumaa Desemba 28, 2018.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa meza kuu na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi na Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Kazi, Vijana, ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Jenista Mhagama na viongozi wengine waandamizi   katika picha ya pamoja na viongoz wa wafanyakazi na wa mifuko ya hifadhi ya jamii baada ya kuwasikiliza hoja zao, kuwahutubia na hatimaye kulipatia jawabu swala la vikokotoo vya wafanyakazi alipokutana nao Ikulu jijini Dar es Salaam leo Ijumaa Desemba 28, 2018. PICHA NA IKULU
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: