Kampuni ya Tanzania Breweries Limited inaungana na mashirika yanayopinga vitendo vya ukatili wa kijinsia na kutetea haki za binadamu katika maadhimisho ya siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia kwa wanawake na watoto kwa kushirikiana na Jeshi la Polisi- Kitengo cha Dawati la Jinsia.

Maadhimisho haya yalioanza wiki iliyopita huandaliwa kila mwaka na Shirika lisilo la kiserikali la WiLDAF kwa kushirikiana na mtandao wa mashirika yanayopinga ukatili wa kijinsia nchini (MKUKI), wadau wa maendeleo na taasisi mbalimbali za kiserikali na za binafsi.

Afisa mawasiliano wa TBL Abigail Mutaboyerwa,amesema mwaka huu TBL itatumia njia mbalimbali kutoa elimu ya uelewa kwa jamii ikiwemo kuendesha semina kwa wafanyakazi wake na jamii katika maeneo mbalimbali kwa kushirikiana na Jeshi la Polisi kitengo cha Dawati. Vile vile wafanyakazi wa kampuni ya TBL wataungana na Polisi pamoja na wadau mbalimbali kushiriki katika kilele cha maadhimisho ya kupinga vitendo vya ukatili wa kijinsia yatakayoandaliwa na Polisi Ilala katika kata ya Kivule ,Wilaya ya Ilala jijini Dar es Salaam Jumamosi tarehe 8 Desemba 2018.
ASP, Fatuma Mtalimbo kutoka Dawati la Jinsia Jeshi la Polisi akitoa mada kuhusiana na ukatili wa kijinsia kwa wafanyakazi wa kampuni ya TDL maarufu kama Konyagi.
Baadhi ya wafanyakazi wa TBL wakifuatilia mada wakati wa semina kuhusiana na ukatili wa kijinsia.

ASP, Fatuma Mtalimbo kutoka Dawati la Jinsia Jeshi la Polisi akitoa mada kuhusiana na ukatili wa kijinsia kwa wafanyakazi wa TBL kituo cha mauzo na usambazaji kilichopo Ubungo jijini Dar es Salaam
Baadhi ya wafanyakazi wa TBL wakifuatilia mada wakati wa semina kuhusiana na ukatili wa kijinsia.
Wafanyakazi wa TDL wakiwa katika picha ya pamoja na afande Fatuma Mtalimbo baada ya semina ya masuala ya jinsia.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: