Mkurugenzi wa Masoko wa Airtel Tanzania, Isaac Nchunda, akizungumza wakati wa uzinduzi wa promosheni ya ‘Dabo Data na Smatika’ itakayomwezesha mteja wa Airtel Money kupata mara mbili ya bando kwa gharama ileile ya sh 2000, Dar es Salaam jana. Kushoto ni Meneja Uhusiano na Mawasiliano wa kampuni hiyo, Jackson Mmbando.

Mkurugenzi wa Masoko wa Airtel Tanzania, Isaac Nchunda, akionyesha bango la promosheni ya ‘Dabo Data na Smatika’ wakatin wa uzindulzi wa promosheni hiyo Dar es Salaam jan, Dabo Data na SMATIKA itamwezesha mteja wa Airtel Money kupata mara mbili ya bando kwa bei ile ile y ash 2000. Kushoto ni Meneja Uhusiano na Mawasiliano wa kampuni hiyo, Jackson Mmbando.
---
Kampuni ya simu za mkononi ya Airtel Tanzania leo imetangaza kuzindua ofa mpya kwa wateja wake inayojulikana kama Dabo Data na SMATIKA ambapo inawawezesha wateja wake wanaotumia huduma ya Airtel Money kupata mara mbili zaidi kila wanaponunua bando kupitia Airtel Money kuanzia leo.

Akizungumza leo jijini Dar es Salaam wakati wa kutangaza uzindua huo, Mkurugenzi wa Masoko Airtel Tanzania Isaac Nchunda alisema kuwa “Promosheni ya Dabo Data na SMATIKA itawafaidisha wateja wetu wanaonunua vifurushi kujipatia bando mara mbili yaani 2GB kwa bei ileile ya Sh 2,000 badala ya ilivyokuwa awali 1GB, vilevile mteja ataweza kudumu na bando hilo la 2GB kwa muda wa siku tatu, Nchunda aliongeza kuwa “kulingana na ripoti ya TCRA ya hivi karibuni inaonyesha kuwa wateja wanaoutumia huduma ya kifedha ya simu za mkononi imeongezeka kutoka 21 milioni Disemba 2017 mpaka kufikia 23 milioni kwa sasa na hii ndio inayotupa msukumo sisi Airtel kuenedelea kuleta huduma za kibunifu kama hizi ili kuwarahisishia wateja wetu kila mahali.”

“Airtel Tanzania bado tunaendelea kuleta huduma na bidhaa ambazo ni nafuu na zenye ubunifu zaidi ili kuendelea kukidhi matakwa ya wateja wetu, aliongeza Nchunda.

Kwa upande wake, Meneja Uhusiano na Mawasiliano wa Airtel Jackson Mmbando alisema kuwa kuzinduliwa kwa huduma hii ya Dabo Data na SMATIKA ni hatua nyingine muhimu ya kuendelea kubadilisha maisha ya wateja wetu. 


‘Tunaona wateja wengi wanaongezeka na kutumia huduma ya Airtel Money. Kuanzia leo, mteja yeyote wa Airtel Money anaweza akanunua bando ya Dabo Data na SMATIKA kwa kupitia menu ya Yatosha *149*99# kisha changua 1 na kuchagua Dabo Data na SMATIKA. Vile vile, mteja anaweza kupiga menu ya Airtel Money moja kwa moja *150*60# kisha akachangua 2, aliongeza Mmbando.


Airtel tunaamini kwa kuwapatia wateja wetu uhuru wakuchagua huduma watakayo kama hivi, inaokoa muda wa mteja kupata huduma haraka na hiyo kuongezea faida kwa mteja kuona thamani ya matumizi ya fedha yake kutokana na unafuu. Kwa sasa mteja atapata mara mbili kwa kutumia Dabo Data na SMATIKA na atalipa kwa Airtel Money yake kuendelea kufurahia huduma zingine za Airtel Money.

“Dhamira ya Airtel ni kuendelea kuwekeza kwenye huduma zetu zote kama ilivyo kwa Airtel Money ambapo hadi sasa Airtel tayari imefikisha huduma za Airtel Money kila kona kwa kusambaza Airtel Money Branch zaidi ya 500 nchini kote, Lengo letu kwa kupeleka maduka haya karibu na wateja zaidi ni kudhihirisha mkakati wetu wa kuwa kampuni ya simu za mkononi ambayo inatoa suluhisho kwenye huduma za kifedha hapa nchini. Nia yetu ni kuendelea kujenga mtandao imara na kutengemea huduma rafiki kama Airtel Money aliongeza Mmbando.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: