Makamu wa Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Samia Suluhu Hassan akifariji Waziri wa Maliasi nac Utalii Tannzania Mhe.Dkt. Hamis Kigwangalla, kwa kufiwa nac Mtoto wake.alipofika kuhudhuria msiba Kijiji cha Puge Nzega. 
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akimpa mkono wa pole JR Hamisi Kigwangalla kufuatia kifo cha mdogo wake Zul, kulia ni Baba wa Marehemu Zul, Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe. Dkt Hamisi Kigwangalla muda mfupi kabla ya mazishi yaliofanyika Puge wilayani Nzega mkoa wa Tabora.
TABORA. Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe.Samia Suluhu Hassan ameongoza shughuli za mazishi ya Zulqarinain mtoto wa Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt.Hamisi Kigwangalla yaliyofanyika leo Ijumaa Februari 22, 2019 saa kumi jioni katika kijiji cha Puge, Nzega vijijini jimboni kwa Waziri Kigwangalla.

Mazishi hayo yamehudhuriwa na viongozi mbalimbali wakiwemo baadhi ya Mawaziri, Manaibu Waziri Wabunge pamoja na Watumishi wa Wizara ya Maliasili na Utalii.

Marehemu Zul alifikwa na mauti jana majira ya saa nne asubuhi JAKAYA KIKWETE CARDIAC INSTITUTE katika hospitali ya taifa ya Muhimbili alikokuwa amelazwa akiwa anasumbuliwa na tatizo la moyo.

#R.I.P Zul.
Inna lillahi wainna illaihi rajiuun
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: