Mwenyekiti wa Bodi ya Utalii Tanzania Jaji Mstaafu Thomas Mihayo akitia saini kwenye karatasi ya makubaliano ya ushirikiano wa maandalizi ya maonesho ya ngumi ya kimataifa yatakayoambatana na Mkutano wa Wafanyabiashara na Watalii kutoka katika mataifa 75 Duniani utakaofanyika mwanzoni mwa mwezi Julai mwaka huu 2019,kushoto kwake ni Makamu wa Rais wa Kampuni ya Rejoy ya China inayoandaa mashindano hayo Bw. Andrew Lu
Mwenyekiti wa Bodi ya Utalii Tanzania Jaji Mstaafu Thomas Mihayo na Makamu wa Rais wa Kampuni ya kimataifa ya Rejoy ya nchini china wakionyesha karatasi za makubaliano ya ushirikiano wa maandalizi ya mchezo wa ngumi wa kimataifa utakaofanyika Jijini Arusha mapema mwezi Julai mwaka huu

Na Grace Semfuko-MAELEZO.

February 22, 2019.

Bodi ya Utalii Tanzania TTB imetiliana saini mkataba wa ushirikiano na Taasisi ya Rejoy ya Beijing Nchini China ya maandalizi ya mikutano mikubwa ya siku mbili ya wafanyabiashara wa sekta mbalimbali wa nchi hizo wakati wa msimu wa maonesho ya kimataifa ya mchezo wa ngumi yanayotarajiwa kufanyika Jijini Arusha mwanzoni mwa mwezi Julai mwaka huu.

Mkataba huo unahusisha maandalizi ya mikutano ya washiriki wa maonesho hayo, ambapo wafanyabiashara na Watalii kutoka katika Nchi zaidi ya nchi 75 Duniani wanatarajiwa kushiriki maonesho hayo yatakayoambatana na kutembelea vivutio vya utalii pamoja na kubadilishana uzoefu wa kibiashara baina ya watu wa mataifa hayo.

Akizungumza mara baada ya kutiliana saini makubaliano hayo, Mwenyekiti wa Bodi ya TTB Jaji Mstaafu Thomas Mihayo, alisema ni hatua muhimu kwa Tanzania ya kupokea ugeni huo ambao pamoja na kunufaisha Taifa kiuchumi lakini pia utatangaza Tanzania katika utalii.

“Sisi Bodi ya Utalii Tanzania ni furaha yetu kuona tumefikia makubaliano haya ambayo yataleta tija kwa Taifa letu, Kampuni ya Rejoy ni ya kimataifa ambayo imepewa idhini ya kuandaa mchezo wa ngumi Duniani, ni kampuni kubwa, maarufu na yenye uzoefu wa kutosha katika mchezo huo, hivyo kuja kwao Tanzania ni hatua kubwa sana,pia Ukumbi wa mikutano Arusha AICC wanahusika katika makubaliano haya” alisema Jaji Mstaafu Thomas Mihayo Mwenyekiti wa Bodi ya Utalii Tanzania TTB

Makamu wa Rais wa Kampuni ya Kimataifa ya Rejoy, Bw. Andrew Lu, ambayo wemekuwepo nchinikwaa wiki sasa, alisema makubaliano hayo yanalenga kuwaweka karibu TTB na Kampuni yake na kwamba watahakikisha maandalizi ya mikutano na mchezo huo wa ngumi yatafanikiwa kwani wameweka hamasa kubwa kwenye nchi zilizoonyesha nia ya kushiriki.

“Tunautangaza mchezo huo kwa hapa Tanzania, watu wengi watakuja kushiriki na kuuona, pia tunatangaza utalii wa Tanzania ili watu hao wakija waweze pia kutembelea hifadhi za utalii na vivutio vya Taifa la Tanzania, tuna uzoefu wa miaka 15 katika kazi hii na tutafanikiwa” alisema Andrew Lu Makamu wa Rais wa Kampuni ya kimataifa ya mchezo wa ngumi.

Makubaliano hayo ambayo mchakato wake unaanza February 22 na kutarajiwa kukamilika machi mwishoni, utekelezaji wake utaanza mwezi April kwa maandalizi ya kupokea ugeni huo mkubwa huku mwezi julai mwanzoni Tanzania ikitarajiwa kupokea ugeni huo kutoka katika mataifa mbalimbali, zaidi ya 70 duniani.

Katika tukio kubwa hilo la ngumi za uzito wote ambalo litarushwa mubashara nchi nying duniani litatizamwa na maelfu ya wahudhuriaji toka china na nchi mbalimbali wakiwaa ni watalii na wafanya baishara kama wasafirishaji na wahudumiaji katika sekta ya utalii lengo likiwa ni kutangaza sekta ya utalii duniani.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: