Na Mwandishi Wetu Mwanza.

MKUU wa Mkoa wa Mwanza, John Mongela kesho anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika mkutano utakao wakutanisha Wanamuziki wa fani mbalimbali waliopo jijini Mwanza.

Mkutano huo umeandaliwa na Umoja wa Wanamuzi Tanzania (TAMUFO) 

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Mwanza leo Rais wa TAMUFO, Dkt. Donald Kisanga (pichani) alisema mbali ya Mongela kuwa mgeni rasmi pia kutakuwa na Mbunge wa Kiteto, Mheshimiwa Koshuma ambaye atakuwa mgeni maalumu.

Akizungumzia mkutano huo Dk. Kisanga alisema ni wa muhimu sana kwa wanamuziki hao kwani kutakuwepo na fursa nyingi.

"Mkutano huu utakaofanyika New Mwanza Hoteli ni wa muhimu sana hivyo nawaomba wanamuzi mbalimbali kufika kwani ni fursa ya pekee" alisema Kisanga.

Kisanga alisema mkutano huo umejaa fursa mbalimbali na kuwa TAMUFO imezialika taasisi mbalaimbali ili kuelezea fursa walizonazo ili kuboresha maisha ya wanamuziki.

Alisema kwamba maandalizi yote ya mkutano huo yamekwisha kamilika.

Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: