Promosheni kubwa ya kampuni ya mawasiliano ya Zantel ya 'Tumia EzyPesa Ushinde' ambayo imezinduliwa mapema mwezi huu inaendelea kushika kasi ambapo watumiaji wake wengi wanaendelea kujishindia zawadi za Simu za kisasa za SmartPhone na inawezesha pia kujishindia fedha taslimu.

Meneja wa mawasiliano wa Zantel, Rukia Mtingwa, amesema kuwa promosheni hii itadumu kwa kipindi cha miezi mitatu na hadi kufikia sasa zimefanyika droo mbili ambazo zimewezesha wateja 60 kujishindia simu za SmartPhone pia kutakuwepo na droo ya mwezi ambayo itawezesha wateja kujishindia fedha taslimu kati ya shilingi 200,000/-mpaka shilingi 1,000,000/-na wateja wapya wanapatiwa motisha.
Meneja wa Zantel kitengo cha Bidhaa EZYPESA Leonard Kameta (kulia) akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya na washindi waliopokea zawadi zao za simu za kisasa za mkononi (SmartPhones).
Mkurugenzi wa Masoko wa Kampuni ya Zantel, Sakyi Opuku akimkabidhi zawadi ya simu mmoja wa washindi wa promosheni ya tumia EzyPesa ushinde, Rehema Ali Rashid wa Mombasa Unguja, hafla iliyofanyika katika ofisi za Zantel Vuga mjini Unguja.
Mkurugenzi wa Masoko wa Kampuni ya Zantel, Sakyi Opuku akimkabidhi zawadi ya simu mmoja wa washindi mshindi wa shindano la tumia Ezypesa ushinde kutoka Zanzibar katika hafla iliyofanyika Zanzibar.
Meneja Uhusiano na Mawasiliano wa Kampuni ya simu ya Zantel Tanzania, Rukia Mtingwa akimkabidhi mmoja ya washindi zawadi ya simu ya kisasa ya mkononi (SmartPhones). Pembeni kushoto anayeshuhudia ni Meneja wa Zantel kitengo cha Bidhaa EZYPESA Leonard Kimeta.
Meneja wa Zantel kitengo cha Bidhaa EZYPESA (kulia) Leonard Kimeta akimkabidhi zawadi  mmoja ya washindi zawadi ya simu ya kisasa ya mkononi (SmartPhones). Pembeni kulia anayeshuhudua ni Meneja Uhusiano na Mawasiliano wa Kampuni ya simu ya Zantel Tanzania, Rukia Mtingwa.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: