Waziri wa ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Isack Kamwelwe akizungumza wakati akifungua mkutano wa DIJITALI KWA MAENDELEO unaokusanya waraghabishi (Infuencers) unaofanyika jijini Dodoma.
Waraghabishi wakifuatilia mkutano huo.
Mbunge wa Hanang Mary Nagu (kushoto) na
Mraghabishi toka Kahama akiuliza swali.
Waziri wa ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Isack Kamwelwe
Mraghabishi Fredy akitoa machache.
Mraghabishi toka Arusha akichangia mada.
Timu ya waraghabishi wa mitandao ya jamii (Social Media Team).
Pichani wa Timu ya waraghabishi wa mitandao ya jamii (Social Media Team) iliyokuwa jijini Dodoma kwa ajili ya kuhabarisha umma.
Serikali imelipongeza Shirika la Oxfam Tanzania kwa juhudi kubwa za kuwafikia wananchi hususan wanawake na kuwawezesha kumiliki ardhi katika halmashauri za Kishapu, Shinyanga vijijini na Hanang’.

Pongezi hizo zimetolewa mjini Dodoma na Waziri wa ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Isack Kamwelwe wakati wa ufunguzi wa mkutano wa siku mbili wa wargabishi ulioandaliwa na Shirika la Oxfam kupitia mradi wa Chukua Hatua.

Akiongea kwa niaba ya Makamu wa Rais Mama Samia Suluhu Hassan, Mhandisi Kamwelwe amesema kuwa Shirika la Oxfam linastahili kupongezwa kwa kazi nzuri ya wanayofanya katika hususan kuwamilikisha ardhi wanawake,

Katika hatua nyingine Waziri Kamwelwe ameupongeza mradi wa Chukua hatua unaoratibiwa na Shirika la Oxfam kwani umekuwa chachu kwa wananchi wa pembezoni kupata huduma ya maji, Barabara, Zahanati na kuwafanya viongozi ngazi ya kijiji, Kata, wilaya hadi taifa kuwajibika.

Awali akitoa taarifa ya Shirika Mkurugenzi mkazi wa Shirika la Oxfam Tanzania Shanty Francis amesema kuwa kupitia mradi wa Chukua hatua wamefanikiwa kuwamilikisha ardhi wanawake 300 katika mikoa ya Geita, Shinyanga na Arusha.

Sambamba na hayo Bwana Francis ameongeza kuwa Oxfam pia imefanikiwa kuwafikia wanawake wanaoishi maisha duni katika kambi za wakimbizi Kigoma kwa kuwasogezea huduma ya maji na huduma zingine muhimu za kijamii.

Mkutano wa wargabishi wa siku mbili ulioanza leo mjini Dodoma umehudhuriwa na watu takribani 200 kutoka mikoa mbalimbali ikiwa ni jitihada za mradi wa Chukua hatua katika kupaza sauti za wananchi waishio pembezoni.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: