Afisa Mradi wa kupinga ukatili wa Kijinsia katika masoko ya Mbagala Rangitatu na Kampochea ujulikanao kama Mpe Riziki si Matusi, Shabani Rulimbiye (kushoto), akitoa mada wakati akitoa mafunzo ya namna ya kujikinga na ukatili wa kijinsia kwa maofisa wa Manispaa ya Temeke jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki.Mafunzo hayo ya siku moja yaliandaliwa na Shirika la Equality for Growth (EfG).
Afisa Ustawi wa Jamii, Getruda Nyagabona (kushoto) kutoka Manispaa ya Temeke akizungumza katika semina ya siku moja ya namna ya kupinga  ukatili wa kijinsia masokoni iliyoandaliwa na Shirika la Equality for Growth (EfG) iliyofanyika mwishoni mwa wiki jijini Dar es Salaam. Kulia ni Afisa Ustawi wa Jamii, Magrida Mumba.
 Washiriki wa semina hiyo wakifuatilia mada kwa makini.
 Mwenyekiti wa Soko la Kampochea, Hemed Said Njiwa akichangia jambo. 
 Majadiliano katika makundi.
 Majadiliano wa kazi za makundi.
 Ofisa Mtendaji wa Mbagala Rangitatu, Morris Ssendi (kushoto), akichangia jambo wakati wa kazi za makundi.
Afisa Ustawi wa Jamii, Magrida Mumba, akichangia jambo.
 Katibu wa Soko la Mbagala Rangitatu, Frank Mapolu akichangia jambo kwenye semina hiyo.
Na Dotto Mwaibale

HALMASHAURI za miji zimetakiwa kuboresha miundombinu ya masoko kwa kuwa yanachangia asilimia kubwa ya pato la Serikali za mitaa nchini.

Ombi hilo limetolewa na Afisa Mradi wa kupinga ukatili wa Kijinsia katika masoko ya Mbagala Rangitatu na Kampochea ujulikanao kama Mpe Riziki si Matusi, Shabani Rulimbiye unaoendeshwa na Shirika la Equality for Growth (EfG) wakati akitoa mafunzo ya namna ya kujikinga na ukatili wa kijinsia kwa maofisa wa Manispaa ya Temeke jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki.

Maofisa walionufaika na mafunzo hayo ni maofisa ustawi wa jamii,maendeleo ya jamii, watendaji wa kata, askari polisi kutoka dawati la jinsia na viongozi `wa masoko.
Alisema masoko mengi ambayo yanaendeshwa na sekta binafsi ambayo imetoa ajira mara tano ya ajira zilizo sekta rasmi na kuokoa wanawake wengi na watoto wao miundombinu yake ni mibovu na hayajawekewa sera na usimamizi wa kisheria kuanzia mazingira ya kazi, kipaumbele kwa makundi maalumu na zaidi ukatili wa `kijinsia `uliokithiri.

"Pamoja na kua ni kimbilio la wahanaga wa mfumo dume, sekta hii pia ni chachu kubwa sana ya maendeleo ya mwanannchi binafsi, serikali za mitaa na Taifa kwa ujumla ambapo takwimu zinaonesha kuwa Halmashauri zinategemea zaidi masoko kwa kuchangia kipato" alisema Rulimbiye.

Aliongeza kuwa pamoja na sekta hii isiyo rasmi kuwa ni chanzo kikubwa cha ajira na kuchangia asilimia kubwa ya pato la Taifa, mazingira yake yanafanywa kama chaka la utovu wa nidhamu na wahanga wakubwa ni wanawake, ambao ni wengi ambao pia wakati mwingine hujumuika na watoto wao.

Afisa Ustawi wa Jamii, Getruda Nyagabona alisema kesi nyingi za ukatili wa kijinsia zimekuwa zikitatuliwa kwa ushiriano baina yao na viongozi mbalimbali kuanzia ngazi ya chini jambo ambalo limesaidia kupunguza vitendo hivyo.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: