Kama tulivyokwisha sikia kwenye chombo chetu cha Mamlaka ya Hali ya hewa Tanzania kuna maeneo ambayo yatakumbwa na kimbunga kilichopewa jina Keneth mapema kuanzia siku ya kesho japo hatujajuwa muda rasmi lakini kinaweza kikawasili hata kuanzia leo usiku.

Tumeona ni jambo jema ku share nanyi jambo hili ili kuokoa maisha na kupunguza madhara yatakayo jitokeza kule kwa wenzetu kusini mwa Tanzania.

Kiukweli kwa mazingira na hali ya kimaisha kwa sisi waTanzania sio rahisi kujikoa na majanga haya ya vimbunga kutokana na aina ya nyumba zetu pamoja na kukosa mazingira au maeneo ya Emergency kwa matukio kama haya au kuhama kwa muda.

JINSI YA KUJIOKOA

Zaidi ya kuhama eneo la tukio Huwezi kuzuia kimbunga hata siku moja na madhara yake huwa ni makubwa sana lakini vipo vitu vichache sana ambavyo ukivifuata vinaweza kukupunguzia madhara ki mwili.

Kimbunga kitawasili na Mvua kali sana yenye upepo mkali kwahivyo baada ya kuona hivyo fuata mambo haya yafuatayo.

1. Kitu cha kwanza usi panic tuliza moyo wako na usiwe na Papara na pia punguza woga.

2. Funga milango yote ya nyumba yako pamoja na madirisha yote usiache wazi hata sehemu moja.

3. Usikae karibu na Madirisha au Milango kwasababu maeneo hayo hayatakuwa si salama kipindi upepo huo mkali unapita.

4. Tunashauri wazazi mkae karibu na watoto wenu kipindi chote ambacho upepo utakuwa unapita.

5. Kama unaishi kwenye nyumba ambayo unahisi haitaweza kuhimili upepo mkali kwa siku ya leo omba hifadhi kwenye nyumba ambayo kuna uwezekano ikahimili upepo mkali.

6. Kuna uwezekano upepo ukaona umeizidi nyumba yako na sasa unataka kuangusha nyumba. Usitoke na kukimbia hovyo. Wewe na watu wako ingieni chini ya kitu kigumu kama vile meza kwasababu utakapo toka nje huku upepo mkali ukiwa unavuma madhara yake huenda yakawa makubwa kwasababu upepo utapeperusha Mabati, miti na vitu vingine ambavyo vikikukuta vinawedha kuleta madhara makubwa.

7. Kuna uwezekano kimbunga kikaleta maji mengi sana na kuanza kujaa ndani. Ikitokea hali hii basi mtalazimika kutoka ndani kwa usalama. Shikaneni mikono na hakikisheni mnatembea pembezo pembezo msitembee maeneo ya wazi kutokana na vitu vitavyokuwa vinapeperushwa vikiwakuta itakuwa ni madhara makubwa. Tembeeni kwa usalama na kwa haraka muwahi sehemu ambayo mtaona itakuwa na usalama.

8. Kama kimbunga kitajaza maji mengi basi ni vema yakaandaliwa madumu matupu kisha yafungwe vizuri yasipitishe hewa yatasaidia kuelea kwa wale ambao watakuwa hawajiwezi kwa kuogelea haswa watoto na wazee.

Mambo hayo kadhaa nimejaribu kupitia katika website mbalimbali kusoma kisha kuwaleteeni hapa.

Kusoma kwa undani zaidi kuhusu kumbunga hiki bonyeza Link hiyo hapo chini.


OMBI

Tunaomba ku share post hii mara nyingi uwezavyo iwafikie wale wote watakaoweza kuiona kwasababu madhara ya kimbunga IDAI kilicho tokea nchi za jirani kusini mwa Tanzania wiki kadhaa zilizopita yalikuwa ni makubwa saana na tuliondokewa na ndugu zetu 960 na zaidi Hakuna mtu aliejuwa kuwa madhara yatakuwa makubwa kiasi kile na mpaka sasa Takribani watu Milioni 3 bado wanahitaji misaada ya kibiinaadamu.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: