Skyline... eneo linalovutia kwa muokenao wake na madhari mwanana. Picha zote na Cathbert Kajuna - Kajunason/MMG.

Watalii wa ndani wakiwa katika skyline.

Muonekano wa milima ya Usambara.
Watalii wa ndani wakiwa katika Jiwe la Mungu...

Eneo la Bwawa lililopo Grewal...
Mashine zilizokuwa zikitumika kupasua mbao.
Mtalii wa ndani akifanya mahojiano na kituo cha ITV.
Furaha.
Muongoza watalii wa Hifadhi ya Asilia ya Magamba Mensieur akieleza machache.
Furahaa.
Nyani aina ya mbega.
Burudani ya muziki wa asilia...
Maporomoko ya maji ya Mvueni.

Na Cathbert Kajuna - Kajunason/MMG.

Katika kuhakikisha tunapata watalii wengi zaidi hifadhi ya Misitu Asilia Magamba imeendelea kuwa kivutio kwa watalii wengi zaidi kutoka ndani ya Tanzania na nje ya nchi.

Hifadhi hiyo imezungukwa vijiji 21 ambapo kati ya hivyo vijiji 17 vipo wilayani Lushoto na vijiji vinne vipo katika Wilaya ya Korogwe imezungukwa na mimea ya aina nyingi, wanyama wengi.

Hayo yamedhihirika hivi karibuni baada ya Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS) kuandaa safari ya watalii wa ndani kutembelea hifadhi ya asilia ya Magamba iliyopo Lushoto na kujionea vivutio mali mbali.

Hifadhi hiyo ina vivutio vingi ambavyo vingine havipatikani kokote zaidi ya kwao ukiwemo Mlima wenye pango la Mjerumani alilolitumia kujificha wakati wa mapigano ya vita ya kwanza ya Dunia.

Akizungumza na wanahabari Mhifadhi Mkuu wa Msitu wa Magamba Bi. Gretuda Nganyagwa amesema kimsingi ndani ya hifadhi hiyo kuna kila aina ya kivuto cha utalii ambapo watakaofika hatachoka kuangalia.

"Hifadhi yetu imekuwa ikitumika kwa ajili ya kufanya mafunzo, tafiti mbalimbali na kubwa zaidi inatumika kwa ajili ya utalii Ikolojia na ndio maana tunatamani kuoana Watanzania wengi wanakuja kushuhudia kwa macho haya ambayo tunayaeleza," amesema.

Alisisitiza ndani ya Magamba pia kuna vinyonga wa pembe mbili, nyani aina ya mbega, kuna wadudu wadogo na wakubwa, wanyama wakubwa lakini ni vigumu kuwaona hadi uende katikati ya msitu, ndege na buibui.

Pia kuna maporomoko ya maji ambayo yanatiriria kwa mpangilio unaovutia, Pango la Mjerumani ambalo lipo kwenye kilele cha mlima ambalo walilitumia kujificha enzi za vita ya kwanza ya dunia.

"Magamba ni hifadhi inayotambulika kisheria tangu enzi za Ukoloni, ina mipaka imara na ndio maana inatambulika kama hifadhi ya Serikali ambayo TFS tumepewa jukumu la kuisimamia. Kadri siku zinavyokwenda idadi ya watalii wa ndani inaongezeka na hivyo kuchangia katika kuongeza pato la nchi yetu,"alisema Nganyagwa.

Ameongeza TFS wanaendelea kutoa hamasa kwa Watanzania kutenga muda ili wafike Magamba kwani ni eneo zuri la kwenda hata na familia kwa kuwa kuna huduma za makambi, kuna maua na watakaokwenda watapata nafasi ya kuimarisha viungo kutokana na kutembea ndani ya hifadhi.

Kwa upande wake Meneja toka Wakala wa Misitu Tanzania (TFS) Shaaban Kiulah amesema kwa sasa wapo katika kampeni ya kuhamasisha Watanzania kujenga tabia ya kutembelea hifadhi za misitu ya asili ambako kuna vivutio vya utalii wa asili.

"TFS tunasimamia hifadhi za misitu ya asili 17 nchini, na hifadhi hizo ziko katika maeneo mbalimbali na kote huko watakaokwenda wataona namna ambavyo Mungu ameipendelea nchi yetu kwa kuweka kila aina ya kivutio cha utalii.Hivyo nitoe rai kwa Watanzania ni wakati wenu kutembelea vivutio vyetu vya utalii, "amesema.

Alifafanua kwa sasa wanakwenda katika msimu wa utalii na hivyo TFS imejipanga kuhakikisha wananchi wenye utayari wa kutembelea hifadhi za misitu ya asili wanapata nafasi hiyo na kuona kila ambacho watatamani kukiona na hasa utalii wa asili.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: