Kamishna Jenerali wa Magereza Phaustine Kasike (wa pili kushoto) akipata maelezo kwa mfungwa anayehusika na upikaji wa chakula Gerezani hapo. Picha zote na Kitengo cha Habari, Makao Makuu.
Kamishna Jenerali wa Magereza Phaustine Kasike (kushoto) akipokelewa na Mkuu wa Magereza Mkoa wa Mwanza Kamishna Mwandamizi Msaidizi Hamza Sadik mara baada ya kutua kwenye uwanja wa Ndege wa Mwanza akitokea Dar es Salaam.
Mkuu wa Magereza Mkoa wa Kagera Kamishna Msaidizi Raymond Mwampashe (kushoto) akimpokea Kamishna Jenerali wa Magereza Kasike( wa kati) mpakani mwa Wilaya ya Chato na Wilaya ya Muleba baada ya Kamishna Jenerali kumaliza maudhurio ya hafla ya uzinduzi wa Hifadhi ya Taifa Burigi-Chato.Kulia ni msaidizi wa Kamishna Jenerali Mrakibu Msaidiza Melkior Komba.
Mkuu wa Gereza la Wilaya ya Muleba, Mrakibu Hadar Yuda(kulia) akimkaribisha Kamishna Jenerali wa Magereza Phaustine Kasike (kushoto) Gerezani hapo. Katikati yao ni Mkuu wa Magereza Mkoa wa Kagera Kamishna Msaidizi Raymond Mwampashe.
Kamishna Jenerali wa Magereza Phaustine Kasike akiweka saini katika kitabu cha kumbukumbu ndani ya Gereza la Wilaya la Muleba.
Mganga wa Gereza la Wilaya ya Muleba, Koplo Diana(kulia) akitoa maelezo kwa Kamishna Jenerali wa Magereza Kasike (wa kati) jinsi anavyowahudumia Wafungwa na Mahabusu wa Gereza hilo. Kushoto ni Mkuu wa Gereza la Wilaya ya Muleba, Mrakibu Hadar Yuda. 
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: