Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na Abiria wa Kivuko cha MV Mwanza na MV Misungwi kuhusu ujenzi wa Daraja litakalopita ziwani katika eneo la Kigongo na Busisi mkoani Mwanza. Mkandarasi wa Daraja hilo anatarajiwa kupatikana ndani ya miezi miwili na Daraja hilo litakuwa na urefu wa kilometa tatu zitakazopita majini. Daraja hilo litagharimu kiasi cha shilingi Bilioni 300.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwapungia mkono abiria wa Kivuko cha MV Mwanza na MV Misungwi mara baada ya kuzungumza nao katika eneo la Busisi Sengerema mkoani Mwanza.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akielekea kupanda Kivuko cha MV Mwanza katika eneo la Busisi wakati akitokea Geita. PICHA NA IKULU
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: