Rais Dkt. John Pombe Magufuli akimshukuru Waziri wa Mambo ya Nje wa Kenya Mhe. Balozi Monica Juma baada ya kukabidhi Dhahabu pamoja na pesa iliyokamatwa Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Jomo Kenyatta jijini Nairobi zikitoroshwa kutoka Tanzania kwenye hafla ya makabidhiano iliyofanyika Ikulu jijini Dar es salaam leo Jumanne Julai 24, 2019

Na Waandishi Wetu.

RAIS Dkt. John Magufuli aipongeza Serikali ya Kenya kwa maamuzi yake ya kuirejeshea dhahabu zenye uzito wa kilo 35.34 zilizotoroshwa nchini Tanzania na Wafanyabiashara wasio waamini kwa njia ya magendo mwaka 2018.

Akizungumza katika hafla ya kukabidhi dhahabu pamoja na fedha taslimu akiwa pamoja na ujumbe wa Mawaziri na Watendaji wa Serikali ya Kenya leo Jumatano (Julai 24, 2019) Ikulu Jijini Dar es Salaam, Rais Magufuli amesema kitendo kilichofanywa na Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta ni cha kizalendo na kimedhirisha urafiki na undugu wa kweli baina yake na Tanzania.

Amesema kuwa Serikali ya Kenya kupita vya vyombo ulinzi na usalama vimefanya kazi nzuri inayodhirisha ushirikiano uliopo kati ya Tanzania na Kenya, na ameeleza kuwa kama kusingekuwepo na ushirikiano huo dhahabu na pesa hizo zilizokamatwa kwenye uwanja wa Jommo Kenyatta nchini humo visingelejeshwa Tanzania.

“Tunaipongeza Serikali ya Kenya kupitia vyombo vya vyake vya ulinzi vilivyofanya kazi nzuri ya kukamata dhahabu kilo 35.34 iliyokuwa imeshavuka kwenye mipaka yetu, na tuwapongeze pia kwa kutunza pesa yetu ambayo ilibiwa Tanzania kwenye Benki ya NMB mwaka 2004, kwa kweli huu ni uaminifu mkubwa” amesema Rais Magufuli

Licha ya kuipongeza vyombo vya ulinzi vya Kenya Rais Magufuli ameshangazwa na ukimya kutaka vyombo vya ulinzi vya Tanzania na hivyo kuvitaka kujitafakari kwa namna dhahabu hiyo ilivyoweza kukamatiwa Kenya na Sio Kwenye uwanja wa ndege wa Mwanza ambapo watuhumiwa walitumia ndege ya ‘Precision Air’ kusafirisha mzigo huo.

“Vyombo vyetu vya ulinzi vipo hapa lazima niviseme, dhahabu iliwezaje kufika Kenya tukashindwa kuwakamata watumiwa wakiwa bado kwenye uwanja wa Mwanza?, hapa lazima vyombo vyetu mjitafakari japo mnafanya kazi kubwa lakini ikiwezekana mkajifunze kwa wenzenu wawape mbinu walizozitumia katika hili” amesema Rais Magufuli.

Katika hafla hiyo, Rais Magufuli pia alimpigia simu ya moja kwa moja Rais Uhuru Kenyatta na kutoa shukrani zake na kumdhibitishia kuwa amepokea mzigo huo na kumpongeza kwa ushirikiano wa Serikali yake kwa Watanzania, ambapo Rais Kenyatta akimuhakikishia Rais Magufuli ushirikiano wa kudumu ambao utachochea zaidi maendeleo kama walivyohaidi na kupewa mamlaka na wananchi.

Naye mjumbe maalumu aliyemwakilisha Rais Kenyatta, Monica Juma ambaye ni Waziri wa Mambo ya Nje wa Serikali ya Kenya amesema Serikali ya Kenya itaendeleza ushirikiano wake na Tanzania katika masuala ya ulinzi na usalama kwa kuwa ushirikiano huo utasaidia kukuza uchumi wa pande zote mbili.

Na kwa upande wake Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Palamagamba Kabudi amesema Kenya na Tanzania ni ndugu tokea ezi na enzi, hivyo Serikali Tanzania itahakikisha kuwa inaendelea kushirikiana na Kenya ili kufanya ushirikiano huo unaleta manufaa kwa wananchi wa nchi hizo.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: