
.jpg)


.jpg)


Mkuu wa Idara ya Chapa na Mawasiliano wa Vodacom Tanzania Yvonne Maruma akizungumza katika Wiki ya Ubunifu Tanzania 2026 ambapo alizungumzia namna ya Vodacom inavyounganisha Watanzania na kuleta tija kupitia Zaidi ya Mtandao: Hususani Watengeneza maudhui na Majukwaa Mtandaoni kwa kuwapa mtandao bora na simu janja zinazo unga mkono ubunifu wao.
Na Mwandishi Wetu.
Ni katika Wiki ya Ubunifu Tanzania (IWTz) 2026
Katika Wiki ya Ubunifu Tanzania (IWTz) 2026, Vodacom Tanzania imeonyesha mchango wa mtandao, ubunifu na ujasiriamali katika kufanikisha Dira ya Maendeleo Tanzania 2050. Tukio hilo limewakutanisha wabunifu, wajasiriamali, watunga sera, wawekezaji, vijana na wadau mbalimbali chini ya kauli mbiu: “Kutoka Matarajio hadi Mageuzi: Kuibua Njia ya Tanzania Kuelekea Ustawi Jumuishi.”
Vodacom imeshiriki katika mjadala kuhusu uchumi wa watengeneza maudhui, maonesho, mikutano na wadau na shughuli za kuelimisha kuhusu usalama wa mtandao.
Akizungumza katika mjadala wa watengeneza maudhui na majukwaa mtandaoni, Mkuu wa Idara ya Chapa na Mawasiliano wa Vodacom Tanzania, Yvonne Maruma, alisema mtandao una thamani zaidi kupitia fursa unazowawezesha Watanzania kuzipata katika elimu, biashara na ubunifu.
Kupitia Vodacom Youth Base (VYB), kampuni inaendelea kuwawezesha watengeneza maudhui kubaki mtandaoni na kukuza shughuli zao za kidijitali. Ushiriki wa Vodacom katika IWTz 2026 unaunga mkono malengo ya Dira ya Maendeleo 2050 kupitia mageuzi ya kidijitali, uvumbuzi na ukuaji wa uchumi jumuishi.


The upcoming opening of a Plaza Premium Lounge in Dar es Salaam marks long-term commitment to elevating Tanzania’s aviation, tourism, and travel ecosystem.
"This expansion directly supports Tanzania's vision to solidify JNIA as a premier regional hub for international business, trade, and tourism. Operating across more than 600 airports in 150 countries and serving over 30 million passengers annually, PPG brings extensive global operational expertise to the market, seamlessly combining international service standards with authentic local elements to create a refined, destination-inspired journey for every traveller.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan akipokea Salaam Maalum kutoka kwa Rais wa Jamhuri ya Watu wa China Mhe Xi Jinping iliyokabidhiwa kwake na Balozi wa Jamhuri ya Watu wa China nchini Tanzania ni Mhe. Chen Mingjian, Ikulu ya Tunguu, Zanzibar tarehe 28 Julai, 2026.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan akizungumza na Balozi wa Jamhuri ya Watu wa China nchini Tanzania ni Mhe. Chen Mingjian, Ikulu ya Tunguu, Zanzibar tarehe 28 Julai, 2026.