Ndg Makamu Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana Bi Tabia Mwita akizungumza wakati wa Ufunguzi wa Semina elekezi ya kimkakati kwa Wasichana Mkoa wa Dar es Salaam.

Mjumbe wa Baraza Kuu la Umoja wa Vijana Taifa Ndg Rose Manumba na Mratibu Mkuu wa Mafunzo hayo akizungumza wakati wa Ufunguzi wa Semina elekezi ya kimkakati kwa Wasichana Mkoa wa Dar es Salaam.
Washiriki Mbalimbali wakifuatilia Mada 
Sehemu ya Meza kuu ikiimba wimbo wa Hamasa Wapili kulia ni Ndg Tabia Mwita Makamu mwenyekiti wa UVCCM, Bi. Rose Manumba Mjumbe wa Baraza Kuu Taifa na Mratibu wa Mafunzo hayo(tatu kulia),(pili kushoto) Bw. Jafari kubecha mgamba (MNEC) anaewakilisha kundi la Vijana pamoja na wawasilishaji mada wakati wa Ufunguzi wa Semina elekezi ya kimkakati kwa Wasichana Mkoa wa Dar es Salaam.
Ndg Rose Manumba akiongoza Mjadala kwa Washiriki.
Ndg Dorris Mollel ambaye ni Mkurugenzi wa Doris Mollel Foundation akiwasilisha mada.
Suma Mwaitenda ambaye ni Mkurugenzi wa FURSA, kutokea Clouds Media Digital akiwasilisha mada
Ndg Jafari Kubecha Mgamba akizungumza wakati wa ufangaji wa Mafunzo maaalum kwa ajili ya wasichana wa mkoa wa dar es salaam (PICHA ZOTE NA FAHADI SIRAJI WA UVCCM)

Makamo wa Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana Vijana wa CCM Taifa Bi. Tabia Mwita amefungua mafunzo Maalum kwa Wasichana kwa Mkoa wa Dar Es Salaam.

Mafunzo hayo Yaliyosimamiwa na kuratibiwa na Mjumbe wa Baraza Kuu la Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi  Bi. Rose Robert Manumba kwa Kushirikiana Taasisi ya Kijerumani FES kwa lengo la kuwaelimisha na kuwaongezea ujuzi na Maarifa yakiuongozi.

Pamoja na kufungua Mafunzo hayo Miongoni mwa waliyotoa na mada ni Bi. Tabia Mwita na amewasilisha Mada ya Ushiriki wa wanawake katika siasa ambavyo amesisitiza wanawake kuendelea kujitokeza kwa wingi kuwania nafasi mbalimbali za kisiasa bila kuogopa. Amewasihi wanawake kujiamini na kutokukubali kukatishwa tamaa. 

Makamu huyo amesisitiza umuhimu wa kuwa na umoja na mshikamano ili kuendeleza kusaidia Serikali katika juhudi zinazofanyika kumuinua Mwanamke.

Aidha, Mjumbe wa Baraza Kuu UVCCM Taifa Rose Manumba akiwa amesisitiza kuwa ni muhimu sisi kama wasichana kuwa sehemu ya mabadiliko tunayotamani kuyaona katika nchi yetu na hata duniani kwa ujumla. Tuwe tayari kutumikia nafasi zetu popote pale tulipo kuendelea kuunga mkono Juhudi za Mhe. Rais Dr. John pombe Magufuli anayepambana usiku na mchana kumuinua mwanamke wa kitanzania ili kuleta maendeleo katika Taifa letu. 

Wameshiriki wakufunzi mbalimbali kama Dorris Mollel ambaye ni Mkurugenzi wa Doris Mollel Foundation aliyewasilisha mada ya Mchango wa asasi za kiraia katika kumuinua Mwanamke Na Suma Mwaitenda ambaye ni Mkurugenzi wa FURSA, kutokea Clouds Media Digital aliyewasilisha mada ya; Namna gani msichana anaweza kuziona na kuzipata Fursa.

Bw. Japhary Kubecha ambaye ni Mjumbe wa Halmashauri kuu ya UVCCM Taifa katika kufunga mafunzo hayo amesisitiza wanawake kujituma katika kazi na sio kuridhika na nafasi mbalimbali ambazo wanaweza kupata kwa kigezo kuwa ni wanawake.

Mafunzo haya yamehudhuriwa na viongozi mbalimbali; Mwenyekiti wa UVCCM Wilaya ya Kinondoni Lilian Rwebangira, Abdul-Rahman Killo na Mwanaidi ambao ni Maafisa kutoka UVCCM Makao Makuu.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: