Blog ya Kajunason inasikitishwa na Vitendo vya Unyanyasaji na Ubaguzi vinavyoendelea nchini Afrika Kusini, maarufu kama 'XENOPHOBIA' dhidi ya Rais kutoka Mataifa mengine wanaoishi nchini humo.

Vitendo hivi vimeripotiwa kutokea katika baadhi ya maeneo katika jiji la Johanesburg na Pritoria, ambapo miongoni mwa waathirika wa vitendo hivyo ni Watanzania wenzetu, ambao baadhi yao wameshindwa kufanya shughuli zao za kujiingiza kipato kwa kuhofia Usalama wao.

"Mbali na kukiuka misingi ya haki za binadamu, vitendo hivyo pia vinatia doa udugu uliopo miongoni mwetu Waafrika ambao kwa mujibu wa historia za mataifa yetu , tumekuwa na mshikamano tangu enzi za kudai uhuru wa nchi zetu,".

"Tunatoa rai kwa mamlaka zinazohusika zifanye jitihada kuhakikisha raia wa kigeni waliopo Afrika Kusini wanakuwa salama na wanakuwa na uhuru wa kufanya shughuli zao kwa mujibu wa Sheria.

Imetolewa na

Cathbert Kajuna
Mwanzilishi na Mwendeshaji
Kajunason Blog.
Septemba 2, 2019.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: