
Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt Jakaya Mrisho Kikwete, akiwa katika siku ya kwanza ya ziara yake ya kikazi ya siku nne mkoani Tabora, ametembelea Kitongoji cha Ipembe, Kata ya Kiloli, Halmashauri ya Wilaya ya Sikonge, akikagua utekelezaji wa Mradi wa Jamii Salama (Safer Communities Project) unaotekelezwa na Taasisi ya Jakaya Mrisho Kikwete (JMKF) kwa kushirikiana na Serikali.
Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt Jakaya Mrisho Kikwete, akikagua zahanati na nyumba mbili za watumishi Kitongoji cha Ipembe, Kata ya Kiloli, Halmashauri ya Wilaya ya Sikonge, mkoa wa Tabora.
Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt Jakaya Mrisho Kikwete, akipatiwa zawadi ya dumu la asali baada ya kukagua zahanati na nyumba mbili za watumishi Kitongoji cha Ipembe, Kata ya Kiloli, Halmashauri ya Wilaya ya Sikonge, mkoa wa Tabora.
Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt Jakaya Mrisho Kikwete, akiwa na kinamama wajawazito na wenye watoto waliojitokeza kwa wingi kupata huduma katika kliniki tembezi ya mradi wa Jamii Salama (Safer Communities Project) unaotekelezwa na Taasisi ya Jakaya Mrisho Kikwete (JMKF) kwa kushirikiana na Serikali. Ameambatana na Naibu Waziri, Ofisi ya Rais–TAMISEMI, Dkt Jafar Seif; Naibu Katibu Mkuu katika Ofisi hiyo, Profesa Tumaini Nagu.
Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt Jakaya Mrisho Kikwete, akiwa akiwagawia mifuko ya uzazi pamoja na vyandarua vyenye dawa kinamama wajawazito na wenye watoto waliojitokeza kwa wingi kupata huduma katika kliniki tembezi ya mradi wa Jamii Salama (Safer Communities Project) unaotekelezwa na Taasisi ya Jakaya Mrisho Kikwete (JMKF) kwa kushirikiana na Serikali. Pamoja naye ni Naibu Waziri, Ofisi ya Rais–TAMISEMI, Dkt Jafar Seif; Naibu Katibu Mkuu katika Ofisi hiyo, Profesa Tumaini Nagu.
Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt Jakaya Mrisho Kikwete, akiwa katika siku ya kwanza ya ziara yake ya kikazi ya siku nne mkoani Tabora, ametembelea Kitongoji cha Ipembe, Kata ya Kiloli, Halmashauri ya Wilaya ya Sikonge, kujionea utekelezaji wa Mradi wa Jamii Salama (Safer Communities Project) unaotekelezwa na Taasisi ya Jakaya Mrisho Kikwete (JMKF) kwa kushirikiana na Serikali.
Katika ziara hiyo ya 13 tarehe Septemba 2026, Dkt Kikwete, ambaye pia ni Muasisi na Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini ya JMKF, alitembelea kliniki tembezi inayohudumia wananchi wa maeneo ya pembezoni kabla ya kukagua Zahanati mpya ya Ipembe pamoja na nyumba mbili za watumishi wa zahanati hiyo..
Uwekezaji huo umelenga kusogeza huduma muhimu za afya karibu zaidi na wananchi ambao kwa muda mrefu wamekuwa wakisafiri umbali mrefu kufuata matibabu, huduma za wajawazito, afya ya mama na mtoto pamoja na huduma nyingine za msingi.
Dkt Kikwete aliambatana na Naibu Waziri, Ofisi ya Rais–TAMISEMI, Dkt Jafar Seif; Naibu Katibu Mkuu katika Ofisi hiyo, Profesa Tumaini Nagu; pamoja na viongozi mbalimbali wa Mkoa wa Tabora na Wilaya ya Sikonge.
Baada ya kukagua kliniki tembezi, zahanati na nyumba za watumishi, Dkt Kikwete alihutubia mkutano wa hadhara uliohudhuriwa na wananchi wa Ipembe na maeneo jirani, akisisitiza umuhimu wa kuendelea kusogeza huduma za msingi karibu na wananchi, hususan wanaoishi katika maeneo ya pembezoni.
Kwa wananchi wa Ipembe, ujio wa zahanati hiyo ni zaidi ya ongezeko la jengo la huduma za afya. Ni mwanzo wa kupungua kwa safari ndefu za kufuata matibabu, kuimarika kwa huduma kwa wajawazito na watoto, na uwezekano mkubwa zaidi wa kupata huduma kwa wakati.
Kwa JMKF, uwekezaji huo unaakisi dhamira kwamba mahali mtu anapoishi hapapaswi kuwa sababu ya kukosa huduma bora za afya. Ipembe sasa inakuwa mfano wa namna ushirikiano kati ya Serikali, taasisi na jamii unavyoweza kugeuza matumaini kuwa huduma halisi zinazogusa maisha ya wananchi.
Kwa furaha na shukrani zao, wananchi wa Ipembe walimzawadia Dkt Kikwete dumu lililojaa asali, zawadi lakini yenye ujumbe mkubwa wa ukarimu, heshima na furaha ya jamii inayoshuhudia huduma za afya zikisogezwa karibu zaidi na nyumbani.









Toa Maoni Yako:
0 comments: