Usaili huo umeleta pamoja vijana wenye vipaji vya kuimba, kucheza, kuigiza, kuchekesha, wanamitindo na ubunifu mwingine mbalimbali, na kuwaleta kwenye jukwaa moja ili waonyeshe kile wanachoweza kufanya mbele ya watazamaji na wataalamu wa tasnia.
Baada ya Dar es Salaam, safari ya kutafuta Nyota Bigi inaendelea Arusha, Dodoma na Mwanza, ambapo vijana wengine watapata nafasi ya kuonyesha vipaji vyao na kuwania nafasi ya kuwa Nyota Bigi wa msimu huu.
Nani ataibuka kuwa Nyota Bigi? Safari bado inaendelea.





Toa Maoni Yako:
0 comments: