Baadhi ya Wachimbaji wa Kokoto wakiendelea na shughuli zao katika eneo  linalodaiwa kuvamiwa na watu hao,ikiwemo uvunjwaji wa sheria za utunzaji mazingira,na utaraibu wa kuchimba kokoto hizo
Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni akizungumza mbele ya Wachimbaji Kokoto  katika eneo la Boko,ambalo linadaiwa kuvamiwa na wananchi huku  wakiendeleza shughuli za uchimbaji bila kufuata utaratibu/sheria. 
Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Mh Daniel Chongolo akiwa na watalaamu wake  wakiondoka kwenye eneo hilo la wachimbaji Kokoto eneo la Boko,mara  baada ya kujionea hali halisi na kuamuru uchimbaji kokoto katika eneo  hilo usitishwe mara moja,mpaka hapo watakapokutana siku ya Alhamisi na  kuamua nini kifanyike.
Mmoja wa wachimbaji Kokoto katika eneo hilo akieleza jambo kwa mkuu wa  Wilaya Mh.Daniel Chongolo (hayupo pichani),aliyefika kujionea halisi ya  eneo hilo

---
Mkuu wa Wliaya ya Kinondoni, Mhe. Daniel Chongolo amekiri kuwepo kwa migogoro mingi ya ardhi kwenye Wilaya hiyo, ambapo amesema migogoro hiyo inaibuka kutokana na kutengenezwa na watu. 


DC Chongolo ametoa kauli hiyo wakati alipotembelea eneo la Uchimbaji Kokoto katika eneo la Boko jijini Dar es Salaam, eneo lililokumbwa na migogoro baina ya Wawekezaji na Wachimbaji hao. 

Akizunguma na Globu ya Jamii na  Michuzi TV, Mhe. Chongolo amesitisha shughuli za uchimbaji kokoto katika eneo hilo mpaka watakapokaa kwa pamoja Novemba Mosi 2018, kati ya  Wachimbaji wa Kokoto,wamiliki wa eneo na Serikali ili kusuluhisha  mgogoro huo ikiwa sambamba na kuangalia namna ya kuendelea au kuacha  shughuli hizo. 

Chongolo amesema katika maeneo hayo ya uchimbaji  watahakikisha yanakuwa na Leseni ya Manispaa, Leseni ya Madini, Cheti  cha TRA, Mazingira, Mikataba kwa Waajiriwa, Malipo ya ushuru wa Madini  kwa Manispaa na usajili katika uzalishaji Madini. "Kwenye haya maeneo ya uchimbaji Kokoto wanachimba kiholela, uharibufu ni mkubwa sana, magari  yanapita juu chini wamechimba mashimo, mvua ikinyesha wanakimbilia  wanajificha kwenye haya mashimo, ikileta madhara kwa watu malalamiko  yote yanakuja kwa Serikali’’, amesema DC Chongolo. 

Kwa upande  wake mmoja wa Wawekezaji katika eneo la Boko, Mwakilishi wa Kampuni ya  Usafirishaji na Uchimbaji wa Kokoto ya Al-Hushoom Evestment, Badi Lema  amedai wao ni wamiliki halali wa eneo hilo, amesema kuna Watu wamevamia  eneo hilo hivyo waliiomba Serikali ifike kwenye eneo hilo kujionea  uvamizi huo. 

Badi amesema licha ya kulinda eneo hilo, Wavamizi  hao wameendelea kuingia kwenye eneo hilo kwa ajili ya kufanya shughuli  za uchimbaji wa kokoto. Hata hivyo moja ya Wananchi wanaofanya shughuli  hizo za Uchimbaji amedai kuwa eneo hilo wamepewa na Wazo, wamedai eneo  hilo walipewa kama Wananchi wa Boko. Pia baadhi ya Wachimbaji hao  wamedai kuwa ruhusa ya Uchimbaji Kokoto katika eneo hilo la Boko  wamepewa na Serikali ya Mtaa.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: