Bango lenye Kauli Mbiu,' HAKUNA NCHI ITAKAYOBAKI NYUMA' ikiwa ni ujumbe wa Kilele cha Maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya Usafiri wa Anga Duniani (ICAD) yaliyofanyika jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki. Picha zote na Cathbert Kajuna - Kajunason/MMG.
Wafanyakazi na wananchi walioungana katika kilele cha maadhimisho ya  Siku ya Kimataifa ya Usafiri wa Anga Duniani (ICAD) yaliyofanyika jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki.
Nderemo na vificho vilitawala katika kilele cha maadhimisho ya  Siku ya Kimataifa ya Usafiri wa Anga Duniani (ICAD) yaliyofanyika jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki iliyopita.
Kaimu Mkurugenzi Mkuu Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania Mbuttolwe Kabeta (wa piku kulia) akipokea maandamano katika Kilele cha maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya Usafiri wa Anga Duniani (ICAD) yaliyofanyika mwishoni mwa wiki jijini Dar es Salaam.
Kaimu Mkurugenzi Mkuu Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania Mbuttolwe Kabeta (wa kwanza kushoto) akipandisha bendera ya Kimataifa ya Usafiri wa Anga Duniani katika Kilele cha maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya Usafiri wa Anga Duniani (ICAD) yaliyofanyika mwishoni mwa wiki jijini Dar es Salaam.
Wakiimba wimbo wa Taifa.
Wafanyakazi na wananchi wakimshangilia Kaimu Mkurugenzi Mkuu Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania Mbuttolwe Kabeta katika Kilele cha maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya Usafiri wa Anga Duniani (ICAD) yaliyofanyika mwishoni mwa wiki jijini Dar es Salaam.

Kaimu Mkurugenzi Mkuu Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania Mbuttolwe Kabeta alisema kuwa Tanzania kama mwanachama hai wa ICAO, imeendelea kutekeleza kwa vitendo kauli mbiu hiyo ili kukuza sekta na kuifanya itoe mchango wake kikamilifu.

Alisema jitihada za TCAA za kuboresha miundombinu pamoja na raslimali watu zimeanza kuzaa matunda. Matokeo mazuri ya ukaguzi uliofanywa na Shirika la Kimataifa la Usafiri wa Anga (ICAO) mwaka 2017 kuhusu uwezo wa Tanzania katika kusimamia na kudhibiti usalama wa sekta ni udhibitisho tosha ambapo matokeo ya ukaguzi yaliyotolewa Septemba 2017 yalionyesha uwezo wa Tanzania wa kudhibiti sekta umeongezeka toka 37.8 (2013) hadi asilimia 64.35 (2017). Alama hizo zinaifanya Tanzania kuwa juu ya kiwango cha wastani wa asilimia 60 kilichowekwa na Shirika hilo.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: