Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akishuhudia wakati mwanafunzi wa Kidato cha Kwanza katika Shule ya Sekondari ya ST. Pamachius Inclusive, Joseph Mtei ambaye hana mikono, alipokuwa akiandika kwa kutumia vidole vya mguu baada ya Waziri Mkuu kuzindua Shule hiyo, Februari 22, 2019. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa na Mkewe Mary wakisoma maandishi yaliyoandikwa kwa kutumia vidole vya mguu na Joseph Mtei ambaye ni Mwanafunzi wa Kidato cha Kwanza katika Shule ya Sekondari ya ST. Pamchius Inclusive ya wilayani Hai, Februari 22, 2019. Kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Dkt. Anna Mgwira na wa pili kushoto ni Waziri wa Elimu, Sayansi na Tekinolojia, Profesa, Joyce Ndalichako. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza wakati alipozindua Shule ya Sekondari ya St. Pamachiwa Inclusive wilayani Hai, Februari 22, 2019. Kulia ni Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu la Arusha, Isaac Amani na wa pili kulia ni Waziri wa Elimu, Sayansi na Tekinolojia, Profesa Joyce Ndalichako. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: