Articles by "ELIMU"
Showing posts with label ELIMU. Show all posts

Mstahiki Meya wa Halmashauri ya Manispaa ya Kibaha Dr Nicas Mawazo amewataka wazazi wa Shule zilizopo Manispaa ya Kibaha kuiga  jitihada zinazofanywa na Shule zingine katika kuimarisha na kuboresha elimu kwenye Shule zao kwa kushirikiana na walimu.

Hayo ameyasema wakati wa kikao na Kamati ya Shule ya Sekondari ya Mwambisi iliyopo Kata ya Kongowe Manispaa ya Kibaha,  iliyofika katika Ofisi ya Mstahiki Meya kwa ajili ya kujadiliana na masuala mbalimbali.

Akizungumza baada ya Kamati hiyo kuwasilisha mapendekezo yao, Mstahiki Meya Dr Nicas ameipongeza Kamati hiyo kwa kazi kubwa wanayoifanya ya kuhakikisha wanafunzi wa Shule yaSekondari Mwambisi wanaendelea kufanya vizuri kwenye mitihani yao.

"Nawapongeza sana Kamati ya Shule kwa jitihada kubwa mnazofanya , Shule zingine wangekuwa wanafuata utaratibu huu unaofanywa na shule yenu tungekuwa tuna matokeo makunwa na jitihada hizi zina maana kubwa na tungekuwa tunafanya vizuri zaidi  hata hivyo zipo baadhi ya Shule zinafanya hivyo na matokeo yao yanakuwa ni mazuri," amesema Dr Nicas.

Ameongeza kuwa, Ofisi ya Mstahiki Meya itaongezea hela ya ununuzi wa mashine ya Photocopy ambapo iliyokuwepo awali imeharibika na kusababisha wanafunzi kushindwa kupata fursa ya kufanya mitihani mara kwa mara kutokana na gharama.

"Ofisi yangu itachangia kiasi cha Tshs 1,500,000/ = kwa ajili ya ununuzi wa Photocopy ili wanafunzi 1080 waliopo katika Shule ya Sekondari Mwambisi iweze kuwasaidia,"amesema Dr Nicas.

Aidha, Mstahiki Meya amesema Manispaa ya Kibaha imejipanga katika kuhakikisha inajenga miundombinu ya kutosha kwa ajili ya wanafunzi wapya na hivyo amewaasa wanafunzi na wazazi kulinda miundo mbinu hiyo ili wanafunzi wengine waje kuitumia.

Naye Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Shule ya Sekondari Mwambisi, Bw. Hamza Omari Duruge amemshukuru Mstahiki Meya wa Manispaa ya Kibaha kwa kukubali kuonana nao pamoja na kuchangia kiasi cha Tshs 1,500,000/= kwa ajili ya ununuzi wa Mashine ya photocopy ambayo iliyokuwepo imeharibika.

Duruge amesema, jambo hilo ni kubwa sana na wao kama Kamati ya Shule wataendelea kusimamia jitihada zinazofanywa na wazazi za kuhakikisha Shule ya Sekondari Mwambisi inaendelea kufanya vizuri kwenye mitihani yake inayokuja kwa kidato cha pili na kidato cha nne.

Katika kikao hicho, Mstahiki  Meya ametoa rai kwa wazazi wote kuwa serikali inayoongozwa na Rais Dkt Samia Suluhu Hassan imeendelea kujenga shule za nsingi na sekondari na Halmashauri inatoa fedha kwa ajili ya kuboresha miundo mbinu ya Shule ikiwemo madawati ya wanafunzi na ukarabati wa baadhi ya majengo.


Halmashauri ya Manispaa ya Kibaha imewataka wanafunzi waliopata nafasi ya kurudi kusoma kupitia mfumo  usio rasmi pamoja fani mbalimbali kutumia nafasi hizo kusoma kwa bidii na kuwa na nidhamu ili waweze kufikia malengo yao waliyojiwekea.

Hayo yamesemwa wakati wa maadhimisho ya Kisomo ya Juma la Elimu ya watu wazima ngazi ya Halmashauri yaliyofanyika tarehe 01/09/2026 katika Viwanja vya Stendi ya zamani vilivyopo Kata ya Mailimoja, Manispaa ya Kibaha.


Akizungumza kwa niaba ya Mkurugenzi, Afisa Elimu Bi Theresia Charles amesema wanafunzi wanatakiwa kuwa na nidhamu , kwa sababu nidhamu katika maisha itakusaidia kukufikisha mbali kwenye malengo yao.

Bi Theresia amewapongeza na kuwataka wanafunzi hao kuwa mabalozi wazuri kwa wenzao waliopo majumbani , waliokatisha shule kwa sababu mbalimbali kurudi shule na kupata elimu hiyo ambapo inatolewa katika shule na vituo ambavyo vipo chini ya serikali.


"Vijana tusitegemee kuajiriwa pekee, bali tutumie mafunzo na ujuzi tunaoupata kujiajiri na kuanzisha shughuli mbalimbali za kiuchumi,”amesema Bi Theresia


Aidha, amewahimiza vijana waliopata mafunzo mbalimbali kuwahamasisha vijana wenzao kujiunga na mafunzo hayo ili nao waweze kupata ujuzi utakaowasaidia kujitegemea na kuboresha maisha yao


Ameongeza kwa kumshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkr Samia Suluhu Hassan kwa kuruhusu wanafunzi kurudi kusoma kwa mfumo usio rasmi  na umeleta mwanga kwa vijana ambapo kwa sasa wanapata elimu na ujuzi bila malipo.

Naye, Afisa Elimu Watu Wazima  Msingi Manispaa ya Kibaha,  Bi. Juliana Francis Mwakatenya amesema MUKEJA ni ambao ni mpango wa Uwiano kati ya Elimu na Jamii na unahusisha watu wazima kuanzia mikaa 19 na kuendelea ambapo wanapata mafunzo ya Kisomo chenye manufaa (KCM) ambapo watu wazima wasiojua  kusoma kusoma, kuandika na kuhesabu hufundishwa na wakati huo hujifunza ujasiriamali na kuendesha miradi mbalimbali ya kisomo cha kujiendeleza (KCK) ili kujikwamua kiuchumi.

Bi. Juliana amesema , kwa mwaka 2026, kuna wanafunzi 57 wa KCM kutoka kwenye madarasa 5 ikiwemo darasa la Gereza la Mkuza na KCK 145 kutoka kwenye vikundi 20 vya MUKEJA.


Hata hivyo ameongeza kuwa, wana wanafunzi 94, wanaofanga mtihani wa kidato cha pili (Qualifying test) na wanafunzi 283 wanaofanya mtihani wa kidato cha nne ( Private candidate) pamoja na wanafunzi 66 wanaopata ujuzi kutoka mradi wa IPOSA ulipo Shule ya Mamlaka.


Maadhimisho hayo yameshirikisha  vikundi mbalimbali vilivyoonesha bidhaa na kazi zao za ubunifu. Kila kikundi kilipata fursa ya kuelezea bidhaa na kazi wanazofanya, pamoja na kutoa ushuhuda kuhusu namna elimu, mafunzo na ujuzi walioupata ulivyowasaidia katika shughuli zao za kila siku na kujikwamua kiuchumi.

Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es salaam Rais Mstaafu Dkt Jakaya Mrisho Kikwete akiwa na Mkuu wa Harvard Kennedy School, Prof. Jeremy M. Weinstein baada ya mazungumzo yao huko Marekani

Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) kimeingia katika mazungumzo ya ushirikiano wa kimkakati na Chuo Kikuu cha Harvard, Marekani, yakilenga kuimarisha matumizi ya Akili Mnemba (AI) katika elimu, utafiti na uchambuzi wa taarifa.

Mazungumzo hayo yalianzishwa na Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Rais Mstaafu Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete, alipokuwa katika ziara ya kikazi nchini Marekani.

Ushirikiano huo unalenga kujenga uwezo wa kutumia AI kwa ufanisi katika kufundishia, kuongeza kasi ya tafiti, na kurahisisha uchakataji wa taarifa nyingi kwa wakati mfupi, eneo ambalo linazidi kuwa muhimu katika vyuo vikuu duniani.

Katika kipindi ambacho taasisi za elimu ya juu zinakabiliana na changamoto na fursa zinazotokana na AI, hatua ya UDSM kuingia katika mazungumzo na Harvard inaonekana kama mkakati wa mapema wa kuhakikisha Tanzania haiwi nyuma katika mapinduzi ya teknolojia.

Akizungumza katika kikao hicho, Dkt. Kikwete alisisitiza umuhimu wa matumizi sahihi na yenye uwajibikaji ya AI, akibainisha kuwa teknolojia hiyo inaweza kuwa nyenzo muhimu ya kuboresha ubora wa elimu na utafiti iwapo itasimamiwa vyema.

Kwa upande wa Harvard, majadiliano yalihusisha viongozi na wataalamu waandamizi, akiwemo Mkuu wa Harvard Kennedy School, Prof. Jeremy M. Weinstein, pamoja na Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Maendeleo ya Kimataifa (CID), Dkt. Fatema Sumar.

Aidha, timu ya wataalamu wa AI kutoka Harvard ilishiriki majadiliano hayo, wakiongozwa na Prof. Sharad Goel, akishirikiana na Dkt. Dan Levy na Dkt. Teddy Svoronos—wote wakiwa na uzoefu mkubwa katika matumizi ya AI katika sera za umma na uchambuzi wa data.

Mazungumzo haya yatafuatiwa na ushirikiano wa karibu wa Wahusika katika Vyuo Vikuu hivi viwili. Chuo Kikuu cha Harvard cha Harvard kimeahidi kusaidiakatika kukijengea uwezo Chuo Kikuu cha Dar esSalaam kwenye eneo hili.

Ushirikiano huu unatarajiwa kufungua ukurasa mpya katika sekta ya elimu ya juu nchini, kwa kuunganisha utaalamu wa ndani na uzoefu wa kimataifa katika matumizi ya teknolojia ya kisasa.
UFAFANUZI WA TET

Taasisi ya Elimu Tanzania (TET) inaushukuru umma kwa kuendelea kufuatilia kwa karibu taarifa mbalimbali zinazozuhusu utekelezaji wa majukumu yake. TET imeendelea kuhakikisha kuwa majukumu yake yote kama yalivyobainishwa katika sheria anzilishi yanatekelezwa kwa ubora na kuwa yanachangia katika kuimarisha juhudi za Serikali ya Awamu ya Sita za kuimarisha utoaji wa elimu na hatimaye kupelekea kuwa na wahitimu wenye ujuzi wa kuajiriwa, kujiari na kuajiri wengine.

Aidha katika kuhakikisha hili, TET imeendelea kupokea maswali, maoni na ushauri kutoka kwa wadau kwa lengo la kuhakikisha kuwa majukumu yake yanatekelezwa kwa kiwango cha juu.

TET imepokea maoni ya mdau yaliyotolewa kupitia mtandao wa kijamii wa JamiiForums kuhusu somo tajwa hapo juu na inapenda kutoa ufafanuzi ufuatao kwa umma:

Utekelezaji wa Majukumu kwa Wakati
Utekelezaji wa Mtaala wa Kidato cha Tano na Sita uliahirishwa kwa sababu ambazo zilibainishwa wazi kwa umma. Aidha, kuhairishwa kwa utekelezaji wa mtaala huo hakukuwa na athari katika ufundishaji na ujifunzaji wa wanafunzi husika. Katika Mwaka wa Fedha 2024/25 TET imesambaza vifaa vya kufundishia na kujifunzia kwa wakati. Aidha, vifaa hivyo pia vimesambazwa katika Maktaba Mtandao ya TET inayopatikana bure kupitia anwani Ol.tie.go.tz. Kazi ya kusambaza vifaa hivi ni endelevu na juhudi za kujazia upungufu pale unapotokea ni endelevu.

Kuhusu Mafunzo ya Walimu
TET inatambua na kuthamini kuwa walimu walioko kazini tayari walipata mafunzo ya muda mrefu yanayojulikana kwa Kiingereza kama Pre-service ambayo yaliwawezesha kuwa na uelewa mkubwa wa maudhui ya masomo wanayofundisha.

Pamoja na mafunzo haya ya awali Serikali inatambua na kuthamini umuhimu wa mafunzo ya mara kwa mara kwa walimu yenye lengo la kuwafanya kuwa wapya na kuwawezesha kwenda na wakati katika mbinu za ufundishaji na ujifunzaji.

Hivyo, lengo la mafunzo yaliyotolewa kwa walimu wa Kidato cha Tano liikuwa ni kutoa uelewa juu ya masuala yaliyoboreshwa katika mtaala wa Mwaka 2023. Ili kuyafanya mafunzo kuwa endelevu, serikali imeanzisha utaratibu wa kutoa mafunzo endelevu ya walimu kazini unaojulikana kama MEWAKA. Mafunzo haya hutolewa katika ngazi ya shule katika siku moja ya kila wiki.

Malipo ya Posho kwa Walimu
TET inatambua mchango na umuhimu wa walimu katika utekelezaji wa mtaala. Hata hivyo ni muhimu kukumbuka kuwa, malipo ya posho huhusisha kuwasilisha taarifa sahihi za kibenki kabla ya kufanyika kwa malipo husika. Kwa bahati mbaya baadhi ya walimu hawakuwasilisha taarifa sahihi na hivyo kupelekea ucheleweshaji wa malipo yao.

Baada ya hili kugundulika, TET ilifanya mawasiliano na walengwa na wahusika walirekebisha taarifa zao na malipo husika yalifanyika. Kwa bahati mbaya, baadhi ya walimu walichelewa kurekebisha taarifa zao na ikapelekea kufikia mwisho wa Mwaka wa Fedha.

Orodha ya walimu ambao malipo yao yalikuwa bado kukamilika ipo na malipo yao yatafanyika mara baada ya taratibu za kiserikali za kufunga na kuanza mwaka mpya wa fedha kukamilika.

TET inawashukuru umma unaofuatilia kwa ukaribu utekelezaji wa majukumu yake. Aidha, tunaendelea kupokea maoni na ushauri kutoka kwa wadau wote. Maoni hayo yatafanyiwa kazi ili kuhakikisha kuwa utendaji wa TET unakuwa wa tija na unapelekea kuwa na matokeo chanya. Kwa maoni na ushauri wasiliana nasi kupitia barua pepe director.general@tie.go.tz

Imetolewa na Kitengo cha Mawasiliano kwa Umma
Taasisi ya Elimu Tanzania (TET)
10 Julai 2025

Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam.

CHUO  Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) kimeutaarifu umma wa Watanzania na kuwaalika wadau wa elimu na maendeleo, kwa ujumla kushiriki katika Maadhimisho ya kumi ya Wiki ya Utafiti na Ubunifu ya UDSM yatakayofanyika kuanzia Juni 9- 11, 2025 katika Viwanja ya Maktaba ya Chuo.

Akizungumza na Waandishi  wa Habari Kaimu Naibu Makamu Mkuu wa Chuo-Utafiti, Prof. Nelson Boniface (Pichani) amesema kuwa Maonesho hayo yanatarajiwa kuhitimishwa Juni 11, 2025 na mazungumzo ya mashirikiano ya kimkakati, kongamano, maonesho na mawasilisho ya watafiti na wabunifu likiwa ni jukwaa la washiriki kupata fursa ya kubadilishana maarifa na ushirikiano.

Aidha, Prof.  Boniface amesema kauli mbiu ya maadhimisho hayo ni: "Kutumia teknolojia ya Dijitali ili kukuza utafiti, ubunifu na ubiasharishaji,".

Ameongeza kuwa miradi mingi itakayooneshwa ni ile ya wanafunzi na Wanataaluma huku akitanabaisha kuwa mtoa Mada Mkuu ni Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Ndege Tanzania (ATCL), Mhandisi Peter Ulanga na Profesa Lilian Kaale Mkurugenzi katika masuala ya Ubunifu UDSM.

Chuo Kikuu cha Dar es Salaam kinatumia fursa hiyo kujipambanua kwa jamii kwa kuonesha shughuli zake za utafiti, ubunifu, huduma kwa umma na ubadilishanaji maarifa kwa kuunga mkono Dira ya  Taifa ya  Maendeleo 2050.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. George Simbachawene akifurahia jambo na wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Kutwa Ingri mara baada ya kuwasili katika Halmashauri ya Wilaya ya Rorya kwa lengo la kuzindua shule hiyo wakati wa ziara yake ya kikazi iliyolenga kukagua na kuzindua utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo mkoani Mara.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. George Simbachawene (kushoto) akipiga makofi mara baada ya kuweka jiwe la msingi katika Ukumbi wa Halmashauri ya Wilaya Rorya wakati wa ziara ya kikazi ya Waziri huyo iliyolenga kukagua na kuzindua utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo mkoani Mara. Aliyevaa kofia ni Mkuu wa Mkoa wa Mara, Kanali Evance Mtambi.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. George Simbachawene (Wa pili kutoka kushoto) akisisitiza jambo wakati akielekea kuweka jiwe la msingi katika Ukumbi wa Halmashauri ya Wilaya Rorya alipokuwa kwenye ziara yake ya kikazi iliyolenga kukagua na kuzindua utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo mkoani Mara. Kushoto kwake ni Mkuu wa Mkoa wa Mara, Kanali Evance Mtambi na kulia kwake ni Mkuu wa Wilaya ya Rorya, Dkt. Khalfan Haule.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. George Simbachawene akizungumza na Wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Kutwa Ingri mara baada ya kuzindua shule hiyo iliyopo katika Halmashauri ya Wilaya ya Rorya wakati wa ziara yake ya kikazi iliyolenga kukagua na kuzindua utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo mkoani Rorya.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. George Simbachawene akimsikiliza Mkuu wa Wilaya ya Rorya, Dkt. Khalfan Haule wakati akifafanua jambo kuhusu Shule ya Sekondari ya Kutwa Ingri kabla ya Waziri huyo kuzindua Shule hiyo iliyopo Halmashauri ya Wilaya ya Rorya.
Mwonekano wa ukumbi wa Halmashauri ya Wilaya ya Rorya uliowekwa jiwe la msingi na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. George Simbachawene wakati wa ziara ya kikazi ya Waziri huyo iliyolenga kukagua na kuzindua utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo mkoani Mara.
Mwonekano wa madarasa ya Shule ya Sekondari ya Kutwa Ingri iliyozinduliwa na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. George Simbachawene alipokuwa kwenye ziara yake ya kikazi iliyolenga kukagua na kuzindua utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo mkoani Mara.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. George Simbachawene akivalishwa skafu na vijana wa Skauti mara baada ya kuwasili katika Halmashauri ya Wilaya ya Rorya kwa lengo la kukagua na kuzindua utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo mkoani Mara.

Na Veronica Mwafisi-Rorya.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. George Simbachawene amezindua Shule ya Sekondari ya Kutwa Ingri huku akiwasisitiza wanafunzi wa shule hiyo kusoma kwa bidii kwa maendeleo yao ya baadae na taifa kwa ujumla.

Mhe. Simbachawene amesema hayo tarehe 2 Oktoba, 2024 wakati wa ziara yake ya kikazi ya kukagua utekelezaji wa miradi ya maendeleo na kusikiliza changamoto za wananchi katika Halmashauri ya Wilaya ya Rorya mkoani Mara ikiwa ni siku yake ya pili ya kukagua utekelezaji wa miradi hiyo ya maendeleo katika mkoa huo.

Waziri Simbachawene amesema Serikali ya Awamu ya Sita chini ya Uongozi wa Rais Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan imetekeleza miradi mingi ikiwemo ya elimu hivyo ili kuunga mkono jitihada za Rais, wanafunzi hao hawana budi kusoma kwa bidii.

Shule nzuri namna hii kujengwa kijijini ni maendeleo makubwa yaliyofanywa na Serikali ya Awamu ya Sita, hivyo ni wajibu wenu ninyi wanafunzi kusoma kwa bidii kwa maendeleo yenu na taifa kwa ujumla,Mhe. Simbachawene amesisitiza.

Ujenzi wa Shule ya Sekondari Ingri umeigharimu Serikali kiasi cha shilingi milioni 584 mpaka kukamilika kwake ambapo inajumuisha madarasa, maabara, chumba cha TEHAMA na Maktaba.

Ujenzi wa shule hiyo umewaondolea adha ya kutembea umbali mrefu kwa wanafunzi hao na kupunguza msongamano wa wanafunzi katika shule waliokuwa wakisoma awali.

Mhe. Simbachawene amewasisitiza wanafunzi na watumishi wa shule hiyo kutunza majengo na vifaa vyote vilivyomo.

Katika hatua nyingine, Mhe. Simbachawene amezindua ukumbi wa Halmashauri ya Wilaya ya Rorya utakaotumika kufanya shughuli mbalimbali kwa maendeleo ya Halmashauri hiyo.

Na Mwandishi Wetu, WHMTH, Arusha.

Halmashauri ya Wilaya ya Ngorongoro imeahidi kuanza kutenga bajeti sambamba na kuwashirikisha katika vikao, mikutano na shughuli nyinginezo Waratibu wa Mfumo wa Anwani za Makazi (NaPA) ngazi ya Wilaya ili kusaidia sekta zote kuona umuhimu wake.

Ahadi hiyo imetolewa na Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Ngorongoro mkoani Arusha, Bw. Thomas Nade wakati akijibu hoja zilizowasilishwa na Waratibu wa Anwani za Makazi Taifa na Wilaya waliofika ofisini kwake tarehe 26 Agosti, 2024 kutoa mrejesho wa zoezi la Uhakiki wa Taarifa za Anwani za Makazi wilayani humo.

Bw. Nade ambaye pia ni Afisa Maendeleo ya Jamii na Mratibu wa TASAF Wilaya ya Ngorongoro, amesema kutokana na umuhimu wa elimu, miundombinu na mfumo wenyewe wa Anwani za Makazi, atahakikisha analifikisha kwenye vikao vya maamuzi ili katika robo ya pili ya mwaka wa fedha itengewe kiasi fulani.
Akitoa taarifa ya maendeleo ya zoezi hilo kimkoa, Mratibu wa Anwani za Makazi Taifa, Mhandisi Jampyon Mbugi amesema licha ya zoezi la uhakiki, usasishaji na usajili kwenda vizuri bado upo umuhimu mkubwa wa Idara za Kisekta kuwashirikisha waratibu wa NaPA kwa kuwa sasa ni zoezi endelevu.

Awali waratibu hao walitembelea Ofisi ya Mtendaji Kata ya Engurosambu Kijiji cha Engurosambu kukagua maendeleo ya Uhakiki ambapo changamoto iliyoainishwa na watendaji hao wa Kata, Kijiji na Mtaa ni upatikanaji wa mtandao na umbali wa boma moja hadi nyingine inayochangiwa na jiografia ya eneo hilo.

Naye Bw. Jasson Kalile, Mtaalamu wa Mfumo wa Anwani za Makazi kutoka wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari na ambaye anasimamia Kata mbili ikiwemo ya Engurosambu katika zoezi hilo, amesema hadi kufikia tarehe 26 Agosti zaidi ya asilimia 70 ya Anwani zilikuwa zimesasishwa.
Waratibu wa Anwani za Makazi Taifa kutoka Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari pamoja na wa Wilaya walipokutana na Mtendaji wa Kata ya Enguserosambu, Kijiji cha Engurosambu na Mtaa wa Engurosambu Halmashauri ya Wilaya ya Ngorongoro, Arusha tarehe 26 Agosti 2024, ili kukagua maendeleo ya zoezi la Uhakiki wa Anwani za Makazi, Usasishaji na usajili wa taarifa za Anwani za Makazi tangu lililopozinduliwa siku ya tarehe 14 Agosti, 2024 katika Mkoa wa Arusha.

Kata hiyo ni miongoni mwa Kata mbili  za Ngorongoro zilizo mpakani mwa Kenya na Tanzania zenye changamoto ya eneo kubwa na mwingiliano wa wananchi wa nchi jirani ya Kenya pamoja na mawasiliano duni ya mtandao wa simu na intaneti.

MKUU wa Mkoa wa Tanga Balozi Batilda Burian akikagua gwaride kabla ya kufunga mafunzo ya awali ya ya Kijeshi kwa vijana wa kujitolea Operesheni miaka 60 ya JKT kikosi cha Jeshi 838 Maramba.
MKUU wa Mkoa wa Tanga Balozi Batilda Burian akikagua gwaride kabla ya kufunga mafunzo ya awali ya ya Kijeshi kwa vijana wa kujitolea Operesheni miaka 60 ya JKT kikosi cha Jeshi 838 Maramba.
MKUU wa Mkoa wa Tanga Balozi Batilda Burian akizungumza wakati alipofunga mafunzo ya awali ya ya Kijeshi kwa vijana wa kujitolea Operesheni miaka 60 ya JKT kikosi cha Jeshi 838 Maramba.
Mwakilishi wa Mkuu wa Majeshi la Ulinzi Tanzania Brigedia Jenerali Abubakari Charo akizungumza wakati wa ufungaji wa mafunzo ya awali ya ya Kijeshi kwa vijana wa kujitolea Operesheni miaka 60 ya JKT kikosi cha Jeshi 838 Maramba.
Mwakilishi wa Mkuu wa Jeshi la Kujenga Taifa Kanali Elias Sikaponda akizungumza wakati wa ufungaji wa mafunzo ya awali ya ya Kijeshi kwa vijana wa kujitolea Operesheni miaka 60 ya JKT kikosi cha Jeshi 838 Maramba.
MKUU wa Kikosi cha Jeshi 838 JKT Maramba Kanali Ashraf Hassan akizungumza wakati wa mafunzo hayo.

Na Oscar Assenga, MKINGA.

MKUU wa Majeshi ya Ulinzi Tanzania Jenerali Jacob Mkunda amesema mafunzo ya awali ya ya Kijeshi kwa vijana wa kujitolea Operesheni miaka 60 ya JKT kikosi cha Jeshi 838 Maramba huku akieleza umuhimu wa vijana hao ni mkubwa kutokana na kwamba wanaingia kwenye Jeshi la akiba ambalo inapotokea hitajiko la ulinzi wa Taifa wanaitwa kwa mujibu wa sheria.

Jenerali Mkunda aliyasema hayo Jumanne Aprili 30 mwaka huu wakati wa ufungaji wa mafunzo hayo ambapo aliwakilishwa na Brigedia Jenerali Abubakari Charo ambapo alisema kutokana na miongozo mbalimbali iliyopo kwa mafunzo hayo ya vijana hasa kwa kuzingatia kwamba vijana hao wanapohitimu mafunzo yao wanaingia kwenye jeshi la akiba.

Alisema kwamba linapotokea hitajiko la ulinzi wa Taifa na Rais na Amri Jeshi Mkuu akatangaza hali ya hatari vijana hao wanaitwa kwa mujibu wa sheria kwenda kuungana na Jeshi la Wananchi (JWTZ) kulinda ulinzi wa Taifa.

Aidha alisema kutokana na umuhimu wa vijana kwenye Jeshi hilo wanapenda kuona wanafikia viwango na malengo ya mafunzo hayo na amewaona wamefikia viwango vinavyotakiwa huku akieleza yanawajenga kwenye nidhamu, ukakamavu, uzalengo, uhodari wa kujiamini na kulipenda taifa lao.

“Nichukue fursa hii kwa niaba ya Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi kutoa shukrani kwa dhati kwa Serikali kwa juhudi zinazofanyika kuhakikisha mazingira ya mafunzo kwa vijana ndani ya JKT yanaboreshwa”Alisema

“Kwani katika mwaka wa fedha 2023/2024 Serikali imetoa kiasi cha sh Milioni 950 kwa ajili ya ujenzi wa mabweni kwa vijana wanaojiunga na JKT fedha hizo zimeweza kujenga mabweni 12 kila moja lenye uwezo wa kuchukua vijana 120 hivyo kusaidia kikosi kuongeza uwezo kuchukua vijana 1440 na hii ni ishara za wazi kwamba serikali inatambua na kuthamini mafunzo ya vijana wa JKT”Alisema

“Lakini pia ujenzi wa vyoo vitano ambapo kila choo kina matundu 22 vitatumika kwa vijana hilo sio suala dogo ni jambo kubwa ambalo serikali imefanya kwa mazingira hayo wanawaomba vijana ambao hawapati fursa kujiunga na JKT wasije kufikiria wametengwa na kunyimwa fursa bali lengo vijana wote wapite Jkt na wale vijana wanaomaliza kidato cha sita”Alisema

Hata hivyo alisema kwamba Jeshi la Kujenga Taifa litakuwa likiendelea kuongozewa uwezo huku akieleza wanathamini juhudi za serikali katika kuboresha mazingira ya jeshi hilo ambapo mafunzo ambayo wameyapata yatawawezesha kuajiriwa kwenye vyombo vya ulinzi na usalama,sekta mbalimbali za serikali au makampuni mbalimbali .

Awali akizungumza wakati akifunga mafunzo hayo Mkuu wa Mkoa wa Tanga Balozi Batilda Burian alisema mafunzo hayo kwa vijana wa JKT ni muhimu sana kwa vijana kwa maana wao ndio tegemeo la Taifa.

Balozi Batilda alisema Rais Dkt Samia Suluhu kupitia falsafa yake ya 4R ameendelea kusimamia na ndio maana juzi chadema walikuwa na maandamano yao wakasimamiwa vizuri na jeshi la Polisi wakafanya mkutano wao wakatembea.

Alisema kwa hakika wakawa na matumaini watapata mambo ya msingi yatakayowasaidia kujenga nchi lakini wakasikia mambo tofauti kwanini wakuu wa mikoa hawapigiri kura, kama madiwani sasa akasema hata RC akipigiwa kura atachaguliwa Tanga na RC ni msaidizi wa Rais anaweza kuhamishwa kila eneo.

“Tulitegemea kwamba hivi sasa nchi ipo kwenye kipindi kigumu na mvua zinanyesha madhara maeneo mengi barabara nyingi zimepata changamoto na maeneo mengi lami zimepasuka changamoto ni nyingi vita vya israel vinaendelea duniani gharama zinapanda bei ya dola ipo kubwa kulingana na bei yetu sisi tukaona haja hoja zao za za kwamba hazikuwasaidia wakapata mawazo mbadala hazipo"Alisema.

Hata hivyo Mwakilishi wa Mkuu wa Jeshi la Kujenga Taifa Kanali Elias Sikaponda alisema kwamba alisema mafunzo hayo ni muhimu kwa sababu yanaleta tija kwa vijana katika shughuli za kujitegemea huku akiwataka kujiepusha na matumizi ya dawa za kulevya.

Aliwataka pia vijana hao kutumia elimu waliyoipata wakaweze kutatua changamoto mbalimbali pasipo kuvunja sheria na taratibu zilizowekwa hapa nchini huku akisiistiza watumie nidhamu pekee kama silaha kwenye jambo lolote mbeleni.
Mratibu wa mafunzo (Supervisor Learning And Development) wa Barrick Tanzania, Elly Shimbi akiongea na Wanafunzi wa Vyuo vikuu wakati wa kongamano la kuwajengea uwezo wa kuhimili ushindani wa ajira na kujiajiri lililoandaliwa na taasisi ya kuchipua na kuendeleza vipaji vya uongozi kwa vijana (AIESEC) lililofanyika katika Chuo Kikuu Cha Dar es Salaam kwa udhamini wa kampuni ya Barrick.

Na Mwandishi Wetu.

Kampuni ya Barrick nchini, imeeleza dhamira yake ya kuendelea kuibua na kukuza vipaji vya vijana wasomi wa vyuo vya elimu ya juu na kati nchini ili waweze kukabiliana na mabadiliko yanayoendelea kutokea duniani na kuhimili ushindani katika soko la ajira sambamba na kuweza kujiamini kutumia ujuzi na taaluma zao kujiajiri kwa ajili ya kujenga mustakabali endelevu.

Hayo yameeleza na Mratibu wa mafunzo (Supervisor Learning And Development) wa Barrick Tanzania, Elly Shimbi akiongea na Wanafunzi wa Vyuo vikuu wakati wa kongamano la kuwajengea uwezo wa kuhimili ushindani wa ajira na kujiajiri lililoandaliwa na taasisi ya kuchipua na kuendeleza vipaji vya uongozi kwa vijana (AIESEC) lililofanyika katika Chuo Kikuu Cha Dar es Salaam (UDSM) kampasi ya Mlimani kwa udhamini wa Barrick ambayo inaendesha shughuli zake nchini kwa ubia na Serikali kupitia kampuni ya Twiga Minerals.

Shimbi, pia aliwaeleza wasomi hao shughuli za kampuni ya Barrick nchini na mkakati wake wa kuinua vipaji vya vijana sambamba na kuwezesha wanafunzi wa kike kusoma masomo ya sayansi ili wapate fursa ya kupata ajira katika sekta ya madini ambayo kwa sasa asilimia kubwa inatawaliwa na wanaume.

Kongamano hilo kubwa limehusisha makampuni mengine makubwa ya ndani na nje kwa ajili ya kuwanoa wanafunzi kuhusiana na mabadiliko ya teknolojia,ajira na kujiajiri wenyewe pindi wamalizapo masomo yao.
Wanafunzi wakifuatilia mada kutoka kwa Watendaji wa makampuni mbalimbali walioshiriki katika kongamano hilo.
Afisa Raslimali wa Barrick Tanzania, Isentruda Mkumba (kushoto) akiongea na wanafunzi waliotembelea banda la maonesho la Barrick kwenye kongamano hilo.
Mratibu wa mafunzo (Supervisor Learning And Development) wa Barrick Tanzania, Elly Shimbi akiwa na viongozi wa AIESEC.
Washiriki wakifanya mazoezi ya kujiweka sawa.