Meneja wa QNET, kanda kusini ya Afrika Biram Fall (katikati) akizungumza na waandishi wa habari wakati wa uzinduzi wa maonesho ya bidhaa za QNET 2019 jijini Dar Es Salaam jana. Wengine kwenye picha ni Mkuu wa Elimu ya Mtandaoni wa QNET Bernie Gaksh (kushoto) na Mshauri wa Biashara wa QNET Tanzania, Edward Mkony.
Mkuu wa Mkoa wa Dar Es Salaam Mhe. Paul Makonda akizungumza na wawakilishi, wafanyakazi na waalikwa wa QNET kuhusu maadili ya kazi kwenye uzinduzi wa maonesho ya bidhaa za QNET jijini Dar Es Salaam.
 Mkuu wa Mkoa wa Dar Es Salaam Mhe. Paul Makonda (katikati) na Meneja wa QNET, kanda kusini ya Afrika Biram Fall (kushoto) wakikata utepe kuzindua rasmi maonesho ya bidhaa za QNET 2019 jijini humo. Kulia ni Mshauri wa Biashara wa QNET Tanzania, Edward Mkony.


Kampuni yenye asili ya Asia ya mauzo ya moja kwa moja QNET imeendesha maonyesho ya bidhaa na huduma zake jijini Dar es salaam siku ya tarehe 16 na 17 Machi 2019. 

Maonyesho yenye jina la Absolute Living, (Kuishi kikamilifu) sambamba na falsafa ya bidhaa za kampuni ya mauzo ya moja kwa moja, huwa yanafanyika kila mwaka katika nchi mbalimbali duniani kote ikiwa na lengo la kuonyesha bidhaa zake na huduma kwenye masoko mapya. Onyesho hilo pia ilikuwa kama jukwaa kwa wateja na wadau wengine wanaotaka kufahamu kuhusu QNET na mtindo wake wa biashara. 

Nadharia ya Absolute Living (Kuishi kikamilifu) inaakisi juhudi za QNET za kukuza mwendendo wa kujali afya, mtindo wa maisha wenye uwiano sahihi, ikiwa inatilia mkazo katika Afya, ustawi na elimu. 

Mgeni rasmi katika hfla hiyo, Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam Mh. Paul Makonda alisema ‘Maisha yangu ni mfano wa kufanya kazi kwa bidi na kujiamini katika kitu chochote unachokifanya. Hii ndiyo njia pekee yakuleta mabadiliko na maendeleo kwa mtu, familia na jamii”. 

Akizungumza kwenye mkutano na vyombo vya habari Meneja Mkuu wa QNET kwa Kanda ya Kusini mwa Jangwa la Sahara Afrika, Biram Fall alisema kwamba, "Tunatoa aina mbalimbali za bidhaa za kiwango cha juu na huduma kwa wateja wetu kuwasaidia waweze kuishi maisha yenye uwiano sahihi, na pia kutatua tatizo la msingi kama vile elimu, ufahamu, na maendeleo binafsi kupitia program za mafunzo yetu, ambayo yanawasaidia katika safari yao ya kujiajiri mwenyewe. Kutoka katika kozi za elimu kwa njia ya mtandao kama vile SELI/qLearn, mpaka katika vifurushi vya sikukuu kama vile Tripsavr, mpaka bidhaa za kuongeza nguvu kama vile Bio Disc3, virutubisho kama EDGE, na saa za mkononi kama Bernhard H. Mayer, QNET ina aina mbalimbali za kukidhi mahitaji mbalimbali ya watu. Katika kitovu cha yote haya, ni hamu yetu ya kutoa fursa ya Kuishi Kikamilifu "Absolute Living”

Zaidi ya watu elfu mbili walipata fursa ya kuona bidhaa za mfano katika onyesho hilo na kufundishwa namna ya matumizi ya bidhaa na faida zake kwa wateja na watumizji wa mwisho. Kwa kuongezea, wataalamu wa bidhaa na biashara walikuwepo kwaajili ya kujibu swali lolote kutoka kwa wageni ili kuelewa vizuri ulimwengu wa QNET. 

Maonyesho ya Dar es salaam yanafuata mfululizo wa maonyesho kama hayo yaliyofanikiwa nchini Togo, Guinea, Ivory Coast, Senegali, Burkina Faso na Cameroon mwaka jana.

Msafara wa maonyesho utasisimama katika mji wa Kumasi, Ghana, baada ya Dar es salaam kuanzia tarehe 23 mpaka 24 Machi mwaka 2019.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: