Mbunge wa viti maalum mkoa wa Iringa kupitia chama cha mapinduzi (CCM) Rose Tweve akihutubia baadhi ya viongozi wa chama cha mapinduzi wa jimbo la Mufindi Kaskazini wakati wa mkutano mkuu wa jimbo hilo.
Baadhi ya viongoziwa chama cha mapinduzi wa jimbo la Mufindi Kaskazini wakati wa mkutano mkuu wa jimbo hilo

NA FREDY MGUNDA, IRINGA.

Mbunge wa viti maalum mkoa wa Iringa kupitia chama cha mapinduzi (CCM) Rose Tweve ameendelea kuitunisha mifuko ya kimaendeleo ya wanawake wa UWT wilaya ya mufindi kwa kukuza mitaji waliyopewa na mbunge huyo.

Akizungumza kwenye mkutano mkuu wa jimbo la Mufindi kaskazini,mbunge Rose Tweve alisema kuwa vikundi vya wilaya ya Mufindi vinajumla ya mtaji wa milioni miambili kumi na nne (200,140,000) ambazo zinatokana na mtaji wa awali ambao mbunge huyo aliwapa.

Ikumbukwe kuwa mbunge Rose Tweve aliahidi kuviwezesha vikundi vyote vya UWT mkoa wa Iringa kwa kila kata akiwa na lengo la kuhakikisha kuwa wanawake wanajikomboa kiuchumi kupitia fedha hizo ambazo alikuwa amewaahidi.

Tweve aliwaomba wanawake wa UWT wilaya ya Mufindi waendelee kufanya kazi na kutunza mtaji huo kwa kuwa ndio mkombozi wa uchumi na amewapongeza kwa kuwa na nidhamu ya fedha ambayo wamekuwa na hadi hapo walipo fika.

“Hongereni sana wakinamama na nawaomba viongozi kuanzia ngazi ya kata hadi wilaya kuendelea kuwalea na kuwapa ushirikiano wa kutosha ili wafikie malengo yawalikusudia kwa kuwa wameonyesha nidhamu ya matumizi ya fedha” alisema Tweve.

Awali mbunge huyo alitoa mitaji ya shilingi laki tano kwa vikundi vya wanawake wa kila kata kama mitaji ya kuanzia biashara zao ambazo zitasaidia kukuza uchumi wa moja moja na wa wilaya kwa ujumla.

Aidha Tweve amewataka Wanawake mkoa Iringa kujiunga katika vikundi mbalimbali vya kijasiliamali bila kujali itikadi za vyama vyao ili kuleta maendeleo.

“Akina mama wasikate tamaa katika kujiunga katika vikundi mbalimbali kwani hiyo inasaidia kubadilishana mawazo katika suala la kutekeleza maendeleo yao” alisema Tweve

Tweve amewataka viongozi kuhakikisha wanawapigania wanawake katika kupata fursa na kuvunja mfumo dume uliopo.

Katika hatua nyingine amewaasa wanawake wanapowezeshwa fedha wahakikishe wanazitumia vizuri ili kufikia malengo yao.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: